SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 7, 2013

VODACOM YAZINDUA ZANZIBAR FASHION WEEK‏

Wanamitindo wakionyesha nguo za asili ya Zanzibar zilizobuniwa na Farouk Abdalah wakati wa Uzinduzi rasmi wa onyesho la Zanzibar Fashion Show Week litakalofanyika tarehe 25, 27 mwezi huu Zanzibar. Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Vodacom Tanzania.

Baadhi ya wanamitindo wakionyesha mavazi wakati wa uzinduzi rasmi wa onyesho la Zanzibar Fashion Show Week litakalofanyika mjini Zanzibar Oktoba 25-27.
 
Mwanamitindo Bula Makia akionyesha moja ya nguo zilizobuniwa na wabunifu wa hapa nchini wakati wa uzinduzi rasmi wa onyesho la Zanzibar Fashion Show Week, litakalofanyika mjini Zanzibar Oktoba 25 hadi 27. Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa  kudhaminiowa na Kampuni ya simu ya Vodacom.
 
Mwanamitindo Pendo Lengo akionyesha vazi lake wakati wa uzinduzi rasmi wa onyesho la Zanzibar Fashion Show Week litakalofanyika tarehe 25,27 mwezi huu Zanzibar.
 
Mmoja wa wanamitindo waliohudhuria katika uzinduzi wa wiki ya maonesho ya Zanzibar Fashion Show, yatakayofanyika Zanzibar akionyesha moja ya vazi katika onyesho lililofanyika jijini Dar es Salaam, kwa udhamini wa Vodacom Tanzania.

0 comments:

Post a Comment