Mke wa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt. Flora Minja(wa kwanza
kulia) akiwa katika hafla fupi ya kuwapongeza Makamishna Wasaidizi
Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa na Mhe. Rais Dkt. Jakaya
Kikwete hivi karibuni. Sherehe za uvalishaji vyeo zimefanyika jana
katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salam(wa kwanza kulia)
ni Mtendaji Mkuu wa Helmet Iniciative Company Ltd, Alpherio Moris ambaye
pia ni Mtaalam Mshauri katika mradi wa uzalishaji wa Kofia ngumu wa
Gereza Kuu Ukonga.
Baadhi ya Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Magereza
wakifurahia katika hafla fupi ya kuwapongeza mara baada ya zoezi la
uvalishaji wa cheo hicho kufanyika katika Viwanja vya Bwalo Kuu la
Maafisa wa Mgereza, Ukonga Dar es Salaam(wa nne kushoto) ni Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Gideon Nkana ambaye pia ni
Mdhibiti Mkuu wa Fedha wa Jeshi la Magereza akifurahia kupandishwa cheo
hicho na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Kikwete kama
anavyoonekana
Baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Magereza wakiwa katika hafla ya
kuwapongeza Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao
wamepandishwa cheo hicho na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja( wa
tatu kushoto) akiwa na Makamishna wa Magereza katika meza Kuu pamoja na
Viongozi Wengine Waandamizi wa Serikali(wa pili kushoto) ni Kamishna wa
Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza kushoto) ni
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili
kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga(wa tatu kulia) ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Dickson Maimu.
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
0 comments:
Post a Comment