Kaimu
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Emmanuel
Mayeji akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua za
utekelezaji wa Program ya Maboresho ya Sekta ya Sheria, wakati wa mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Farida
Khalfan akieleza kwa waandishi wa habari (MAELEZO) mpango wa serikali wa
kuongeza fursa za upatikanaji na utoaji wa haki kwa wote, wakati wa mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam.Kulia ni
Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.
Picha na Fatma Salum
Picha na Fatma Salum
****
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Wizara
ya Katiba na Sheria inatekeleza na kuratibu Maboresho ya Sekta ya Sheria chini
ya Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo ili kuboresha na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma za kisheria za
usimamiaji na utoaji wa haki kwa wote na kwa wakati.
Lengo
la programu hii ni kuboresha miundombinu iliyopo na kuongeza fursa za
upatikanaji na utoaji haki kwa wananchi wote hasa wanyonge.
Maboresho
haya yamejikita katika maeneo makubwa matatu moja ni kuongeza ufanisi na
kusimamia ubora wa huduma ya kutoa haki kwa wote. Nia kubwa ya Serikali katika
lengo hili ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi ili kuongeza ufanisi wa
kusimamia utoaji wa huduma za kisheria na kusimamia haki nchini, ili kutekeleza
lengo hili kuna mikakati iliyopangwa
ambayo ni kuboresha miundombinu ya majengo na mifumo ya kupokea na kutunza
kumbukumbu na nyaraka za mashauri katika idara ya Mahakama hasa Mahakama
Kuu.
Eneo lingine katika uboreshaji wa sekta ya
sheria ni kuboresha ujuzi na kuimarisha taaluma ya Uanasheria nchini. Serikali
ina lengo la kuboresha taaluma ya sheria inayotolewa kwa wanafunzi wa sheria
hasa elimu ya vitendo ili kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati. Ili kutimiza
lengo hili Serikali imejenga chuo cha Uanasheria kwa vitendo na kuweka miundombinu ya kudumu pamoja na
vitendea kazi vitakavyosaidia ufundishaji wa vitendo kwa wanafunzi hao ikiwemo
mahakama.
Serikali pia imeongeza wigo na kuboresha
mazingira ya fursa za upatikanaji wa haki nchini kwa kuboresha mazingira ya upatikanaji
wa haki kwa wananchi wote kwa kusogeza huduma za kisheria karibu na wanannchi
kwa kujenga mahakama za mwanzo na kuanzisha chombo cha kuratibu huduma za
msaada wa kisheria wa wananchi wasiokuwa na uwezo.
Aidha,
tangu kuanzishwa kwa programu hii mafanikio mbalimbali yamepatikana yakiwemo,
kutenganishwa kwa shughuli za upelelezi na zile za uendeshaji wa mashitaka,
kuanzisha ofisi za Mkurugenzi wa Mashitaka Mikoani na Wilayani ambapo hadi sasa
ofisi hizo zipo katika Mikoa kumi na tano na Wilaya kumi na saba.
Mfumo
wa usafirishwaji wa mahabusu na
wafungwa, Ukarabati na ujenzi wa Mahakama 10 katika ngazi mbalimbali na
uanzishwaji na ujenzi wa Taasisi ya
Mafunzo yaUanasheria kwa vitendo ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana
kupitia programu hii.
Mbali
na mafanikio hayo kuna changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji
wa programu zikiwemo ucheleweshwaji wa utolewaji wa fedha kwenye mfuko wa
pamoja kwa upande wa wadau wa maendeleo na Serikali kushindwa kutimiza ahadi
kwa wakati na kwa kiasi kilichokubaliwa.
Kwa
kiasi kikubwa Serikali inajitahidi kuboresha miundombinu na mifumo yake ya
kiutendaji kwa lengo la kutoa huduma bora za utoaji haki kwa wananchi wake. Pia wanachi wanahimizwa
kutafuta haki zao pale wanapoona wanaonewa.
Imetolewa na:
Wizara ya Katiba na Sheria,
Oktoba 07, 2013
0 comments:
Post a Comment