Habari hizo zinapasha kwamba msanii maarufu wa Hip Hop nchini,Albert Mangwair (Mangwea) amefariki dunia nchini Afrika Kusini katika hospitali ya Helen Joseph ya jijini Johanesburg alipopelekwa baada ya kugunduliwa na wenzake asubuhi kwamba alikuwa hoi. Hali hiyo ilimkuta maeneo ya Brixton-Mayfair West ambapo alikuwa amefikia kwa rafiki yake ambaye walisoma wote miaka ya nyuma.
BC imeweza kuthibitisha Exclusively kabisa kwamba ni kweli Ngwair amefariki dunia. Chanzo cha uhakika kutoka Afrika Kusini ambacho BC imeongea nacho kinasema kwamba Ngwair alikuwa asafiri leo kurudi Dar. Lakini asubuhi wenzake walipokwenda kumwamsha walimkuta yeye na mwenzake M to the P wakiwa wamelala bila kujitambua.Juhudi za kuwafikisha hospitali zilifanyika lakini Ngwair ndio akawa ameshaaga dunia. Mwenzake M to the P bado yupo hospitali na hali yake bado ni mbaya.
Kwa mujibu wa chanzo hicho na kwa mujibu wa maelezo ya awali ya Daktari, inaonekana kwamba jamaa walitumia aina fulani ya madawa ambayo bila shaka yaliwazidia (overdose). Uchunguzi kamili wa kitabibu bado unaendelea.
Inasemekana jana jioni alikutana Bar fulani na watanzania wengine takribani 20 hivi na ikatokea kwamba wakawa wanawataja wasanii wengine wa Bongo waliotangulia mbele za haki na kila lilipotajwa jina la msanii aliyefariki, Mangwea yeye akawa anajibu OMG!
Albert Mangwair akiwa na M to the P ambaye bado yupo hospitali. Hali yake inatajwa kuwa mbaya.
Mangwair na Hamisi wakiwa mtaani maeneo ya Brixton – Mayfair West, J’burg, Afrika Kusini
Marehemu Albert Mangwair akiwa na mshikaji Hamisi, Jumamosi hii siku ya Fainali ya UEFA kati ya Bayern Munich na Borusia Dortmund. Ngwair alishabikia
CHANZO: BONGOCELEBRITY
*********
*********
G-SENGO
Ni vigumu kuamini lakini taarifa ambazo tayari zimethibitishwa kwa masaa sasa ni kwamba Rapper, Freestyler, Albert Mangwea amefariki dunia leo hii katika majira ya saa 9 alasili.
SIKILIZA KILICHO SEMWA
HAPA:-
(BOFYA PLAY)
Taarifa zaidi endelea kupitia mtandao huu kila mara.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
*********
*********
WAVUTI
[Update, audio] Tanzia: Mwanamumziki Man Ngwair
MSANII maarufu wa nyimbo za 'hip hop' na Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Man Ngwair aka Ngwair ametangazwa kuwa amefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg.
Kwa mujibu wa taarifa za redio mbalimbali jioni hii nchini, inadhaniwa huenda Ngwair amefariki dunia kutokana na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya. Aidha, taarifa kutoka kwa mmoja wa mtu wa karibu wa Ngwair nchini humo,
Hussein Original aliyepo mji wa Pretoria, alisema alikutwa amefariki wakati msanii mwenzake ‘M To The P’ alikutwa amepoteza fahamu majira ya asubuhi walipokwenda kuwagongea mlango gheto kwao.
Daktari tayari alishathibitisha taarifa hizo na tayari ametoa taarifa kwa watu wa karibu wa msanii huyo.Akiongea na redio ya Clouds FM, mwenyeji mwingine wa Afrika Kusini aliyejitambulisha kwa jina la Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka: “Sijui hata huko alitumia nini,” amesema Johnson.
Amesema naye asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka Ngwair hospitali kwa kuwa alikuwa bado hajaamka.
Taarifa za awali za kifo cha Mangwair - CloudsFM
Naye mwanamuziki Bushoke anayeishi jijini Pretoria amesema alikuwa akutane na Ngwair leo jijini Johannesburg lakini alishangaa kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washikaji ambao ni wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki: “Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke.
Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.
Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.
Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.
Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.Mwaka 2010,
Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili,
Nge.
Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi’.
Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz.
Pumzika kwa amani. Mbele yako, nyuma yetu Ngwair. RIP.
---Imenukuliwa kutoka blogu za Habari Mseto na Bongo Staz
Source: http://www.wavuti.com/
********
*********
DJ FETTY
HIKI NDICHO KILICHOMUUA NGWEA
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Rapper Ngwea, aliejitambulisha kwa jina la Hamisi, amesema Ngwea alikua kule kwa mualiko wa kufanya show South Africa, ambapo alikua na msanii mwingine anaeitwa M to the P, na walitakiwa kuondoka leo kurudi Dar saa tatu asubuhi, lakini baada ya kuona hawatokei ndio wakaamua kwenda walipokuwa wamefikia na kuwakuta wote wawili wakiwa hawajielewi baada ya kujidunga madawa ya kulevya mengi (overdose), walipowahishwa hospitali, habari ndio ikawa hivi, kuwa Ngwea amefariki na M to the P yuko hoi hospitali
May God give you peace brother.
DJ FETTY
********
*********
GLOBALPUBLISHER
MAMA NGWAIR: MWANANGU ALINIAHIDI
KURUDI IJUMAA ILIYOPITA
Marehemu Albert Mangwair enzi za uhai wake.
Akiongea kupitia kipindi cha Amplifire cha Clouds FM, kutoka mkoani Morogoro, mama mzazi wa msanii Albert Mangwair aliyefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini, amesema kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na marehemu ilikuwa wiki mbili zilizopita ambapo Mangwair alimwambia kuwa mzima na anaendelea vizuri na kwamba angerejea nchini Ijumaa iliyopita.
Aliongeza kuwa taarifa za kifo cha mwanaye amezipata jioni hii kwa masikitiko. Wakati Mangwair anaelekea Afrika Kusini hakumuaga mama yake japo akiwa huko alikuwa anawasiliana naye. Kuhusu taarifa za mazishi mama Mangwair amesema bado anasubiri shemeji zake wafike ili wapange.
Mungu ampumzishe Mangwair mahali pema peponi. Amen!
UPDATE ZA GLOBALPUBLISHER HIZI CHINI ZA MWANZO:
M2 THE P ALIYEPELEKWA HOSPITALI PAMOJA NA MANGWAIR NAYE YUPO HOI
BREAKING NEWS: ALBERT MANGWAIR AAGA DUNIA
RIP ALBERT MANGWAIR
NGOMA ALIZOTESA NAZO MANGWAIR
GPL
********
*********
TEENTZ.COM
UPDATE 3: BREAKING NEWS KUHUSU KIFO CHA NGWEA/ LINGINE LILILOTUFIKIA HIVI PUNDE KUUSU M2-THE-P
UPDATE 3: chanzo chetu cha habari kinatupasha kua marehemu Albert Mangwea alikua na msanii mwenzake wa bongo flavor ajulikanae kama M2-THE-P miongoni mwa wasanii waliokuwa marafiki wa kundi la CHAMBER SQUAD,
Habari zinasema kua M2-THE-P nae hali yake sio nzuri na yuko mahututi katika chumba maalumu (I.C.U) ambapo madaktari wamethibitisha kua matumaini ni hafifu ya uhai wa M2-THEP pia..
"hali yake sio nzuri, tumemuwekea mashine ya kupumua na yuko kwa uangalizi wa kina kwa muda wa masaa sita nbaada ya hapo tutaweza kusema nini hatima yake kwa sasa ni hayo tu" - Daktari amenukuliwa..
..endelea kua nasi ambapo tutakujuza zaidi kwa yakini nini sababu ya kifo cha mangwea na nini kimemkumba M2THE-P na alikua na ngwea mpaka mauti yanamfika.....
HABARI HIZI NIMEZINUKUU KUTOKA BLOGS/VYANZO TOFAUTI TOFAUTI ILI KUWEZA KUPATA UHAKIKA WA HABARI YA MSIBA HUU.
SHUKRANI KWA WANABLOG HAWA.
0 comments:
Post a Comment