Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kushoto) akimkabidhi bwana Bernard Chezue modem baada ya kuibuka mshindi wa droo ya kila siku inayowawezesha wateja wa Airtel waliofanya malipo ya bidhaa katika viwanja vya Sabasaba kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku. Akishuhudia ni mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Monica Mgalwa.
Mshindi wa droo ya kila siku ya Airtel money bwana Frank Joakim Mgumba akijaribu kutumia simu yake mara baada ya kuibuka mshindi katika droo inayohusisha wateja wa Airtel walionunua bidhaa kwa kupitia Airtel money katika maonyesho ya Sabasaba. Pichani Katikati ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde pamoja na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja wa viwanja vya Sabasaba.
Mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Monica Mgalwa akichezesha droo ya kuchagua mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kila siku iliyofanyika jana katika viwanja vya Sabasaba ambapo wateja watano walionunua bidhaa kwa kupitia huduma ya Airtel money walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo simu, modem na muda wa maongezi. Wakishuhudia pichani ni wafanyakazi wa Airtel.
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya kila siku Bw Rucha Selemani modem baada ya kuwa mmoja kati ya washindi wa siku wa droo hiyo inahusisha wateja waliofanya malipo ya bidhaa kupitia Airtel money katika viwanja vya Sabasaba kuweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku. Akishuhudia ni mfanyakazi wa huduma kwa wateja wa Airtel bi Heleni Kimati.
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Neema Academy iliyoko jijini Dar es Salaam wakipata maelekezo kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali kutoka kwa watoa huduma wa Airtel mara baada ya kutembelea banda la Airtel lililopo katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba.
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Neema Academy iliyopo jijini Dar es Salaam wakipata maelekezo kuhusu huduma ya internet ya 3.75G kutoka kwa mfanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja baada ya kutembelea banda la Airtel lililopo katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba.
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Neema Academy iliyopo jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea banda la Airtel lililoko katika maonyesho ya Sabasaba kilwa Road jijini Dar es Saalam.
0 comments:
Post a Comment