Mkurugenzi wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi wa harambee hiyo.kushoto meneja rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.
Mgeni rasmi wa harambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa kampuni ya Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma baada ya kuchangia sh. milioni 22.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja (katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya kuchangia sh. 500,000.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Fedha hizo zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400 zilipatikana.
.Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo,wakiongozwa na Waziri Mstaafu Edward Lowassa(wa Pili Kulia) na Meya Wa Ilala Jerry Silaa
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata hiyo Bonah Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi kuingia ukumbini.Picha Zote na Dotto Mwaibale
---
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na matatizo hayo katika shule mbalimbali.
---
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendeleza kuwa mstari wa mbele katika harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya kuchangisha Sh.421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo juzi katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam ambapo yeye mwenyewe alichangia Sh.milioni 10.
Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa ni Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22, African Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja alichangia milioni Sh.10.
Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh. milioni 12.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa jitihada zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani wengine kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwaupande wake alisema shule saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na matatizo lukuki ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja.
. “Shule za kata yangu kwa kweli zinakabiliwa na changamoto nyingi, kwa mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane wakati wanafunzi waliopo ni 2,200, Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15 kilichangwa na wadau mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3 zilitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group ambao walitoa shilingi milioni moja na wanafunzi kadhaa wa shule za msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na matatizo hayo katika shule mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment