Wakulima wa zao la kurosho wapatao 2000 wamejitokeza kwa wingi katika ofisi za bodi ya Korosho jijini Dar es Salaam wakiandamana kuishindikiza bodi hiyo kuwalipa mafao yao ya mapunjo takribani milioni 10 kila mmoja.
Akizungumza na Moblog jijini leo mjumbe wa wakulima hao Ramazani Ngaleni amesema wanaidai serikali mafao hayo kwa muda murefu ambayo hivi sasa imefikia miaka 5 bila ya mafanikio yeyote yale ya msingi.
Moblog ilijitaidi kudodosa zaidi juu ya viongozi wa bodi hiyo lakini jitihada za kuwapata zilishindikana kutokana na kutowepo ofisini leo, na mmoja wa wakulima wa korosho mkoani Pwani Stumai Mohamed amemuomba rais kikwete kuwasaidia ili waweze kulipwa fedha zao kama ilivyoamuliwa na mahakama.
Chini ni picha za wakulima wa korosho wakiwa ofisi za bodi ya korosho jijini Dar-es-salaam, polisi kwenye tukio kama kawa.
Picha zote na Geofrey Mwakibete (Mo blog)
0 comments:
Post a Comment