Mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza hayupo pichani. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kushoto)akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo.Katikati ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kushoto)akimsikiliza Mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo(kulia)Baada ya kukabidhiwa rasmi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 na Mkurugenzi huyo,Katikati ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya Mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo,kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza hayupo pichani,Jumla ya Milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wapili toka kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani,wakati wa kumkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo watatu.kulia ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox,kushoto Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Biashara Mwamvita Makamba. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari wakifatilia makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 kwa mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo.aliyokabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.Jumla ya Milion 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA
.
.
-----
Askari Polisi Ashinda Milioni 10 za M-PESA
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imemkabidhi hundi mshindi wa zawadi ya kitita cha Shilingi Milioni Kumi wa droo ya mwezi ya promosheni ya M-PESA Bw Peter James Kilalo.
Bw. Kilalo amekabidhiwa hundi hiyo leo jijini Dra es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacoim Tanzania Bw. Rene Meza katika hafla fupi iliyohudhuriwa pia na waandishi wa habari.
Akipokea hundi yake Bw. Kilalo ambae ni Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Dar es salaam ameshukuru kw akuibuka mshindi jambo ambalo amesema hakulitegemea.
"Kwa kweli mimi ni mteja mzuri sana wa M-PESA lakini kweli sikutegemea kwamba ningeibuka mshindi, ila sasa ninapopokea hundi hii naamini kwamba nimeshinda na fedha hizi Milioni kumi ni zangu"Alibainisha Bw. Kilalo.
Alipoulizwa namna alivyojipanga kutumia pesa hizo Bw Kialalo alijibu" Jamani mimi ni masikini na sikuwahi kuota kwamba ipo siku nitashinda kiasi kikubwa cha fedha namna hii hivyo jambo kubwa kwangu kwa wakati huu ni kwanza kuacha akili yangu itulie kabisa ndio niamue niziwekeze wapi ili zinikwamue kimaisha"Alisema
"Nina mawazo kadhaa ya biashara ambayo nimekuwa nikiyawaza kama njia ya kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha hivyo hizi pesa nitazielekeza huko ila baada ya akili yangu kwanza kutulia kutoka katika hali ya furaha niliyonayo sasa."Aliongeza
Mshindi huyo ametumia pia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutumia huduma ya M-PESA kwa kuwa mbali na kwamba imerahisisha maisha katika utumaji na upokeaji fedha mijini na vijijini bado wanaweza kuwa katika nafasi ya kushinda kama yeye
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema promosheni hiyo imelenga kuwawezesha wateja wa M-PESA kubadili masiha kutokana na wanavyotumia huduma hiyo.
"Promosheni hii tulizindua mwezi uliopita tukilenga kuwawezesha wateja wetu kujishindia zawadi za fedha taslimu, kiasi cha Shilingi Milioni 480 kinashindaniwa ambapo hadi sasa wateja zaidi ya 4,000 wameshajinyakulia zaidi ya Shilingi Milioni 120" Alisema Bw. Rene
AmesemaVodacom inatambua umuhimu wa huduma ya M-PESA katika maisha ya kila siku ya wananchi na hivyo wakati wote imekuwepo mikakati imara ya kuiwezesha huduma hiyo kuendelea kuwa bora zaidi,salama na ya kuaminika sokoni.
"Matumizi ya huduma ya M-PESA hapa nchini yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana, kiwango cha wananchi kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo ya bidhaa mbalimbali kupitia M-PESA ni kikubwa jambo ambalo linakuwa rahisi zaidi kutokana na mtandao mpana tulionao wa mawakala wanaofikia 20,000 mijini na vijijini." Aliongeza Bw Rene
Promosheni hiyo itadumu kwa siku tisini kutoka Februari 13, 2012 hadi May 13, 2012. Mbali na kutoa mshindi mmoja wa shilingi milioni kumi kila mwezi pia kila siku washindi mia moja hujishindia Shilingi 50,000 kila mmoja.
"Matumizi ya huduma ya M-PESA hapa nchini yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana, kiwango cha wananchi kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo ya bidhaa mbalimbali kupitia M-PESA ni kikubwa jambo ambalo linakuwa rahisi zaidi kutokana na mtandao mpana tulionao wa mawakala wanaofikia 20,000 mijini na vijijini." Aliongeza Bw Rene
Promosheni hiyo itadumu kwa siku tisini kutoka Februari 13, 2012 hadi May 13, 2012. Mbali na kutoa mshindi mmoja wa shilingi milioni kumi kila mwezi pia kila siku washindi mia moja hujishindia Shilingi 50,000 kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment