Benki ya Dunia imetangaza majina matatu ya wagombewa watakaoshindana katika kuwania nafasi ya kuchukua uongozi wa taasisi ya fedha duniani kutoka nchi za Nigeria, Marekani na Colombia.
Wakurugenzi wa bodi ya benki hiyo wanatarajiwa kuwahoji Mmarekani Jim Yong Kim, Mkolombia Jose Antonio Ocampo na Mnigeria Ngozi Okonjo- Iweala na hatimaye kuwapigia kura tarehe 21, mwezi ujao.
Katika kipindi hichi ambapo mataifa yaliyoendelea yakijaribu kushirikiana na Benki ya Dunia, uteuzi wa Okonjo- Iweala na Ocampo kwa mara ya kwanza, unatoa changamoto kwa Marekani ambayo hutoa marais wa taasisi hiyo kila wakati.
Ikulu ya Marekani inampigia kura Kim, mzaliwa huyo wa Korea kushika nafasi ya Robert Zoellick, mwanadiplomasia mkongwe wa Marekani ambaye anamaliza muda wake tarehe 30 mwezi Juni, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment