Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar matokeo ya kufutwa kwa mitihani kwa baadi ya Skuli kutokana na kufanya udanganyifu.mkutano huo umefanyika Hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akionesha ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Uchunguzi ya Vyombo vya Usalama kuhusi undanganyifu wa baadi ya miandiko iliotumika katika mitihani ya watahiniwa wa Kidatu cha Nne.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Matihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichoka, akionesho karatasi za mitihani ambozo zimekuwa na miandiko zaidi ya mmoja na kufanana maneno ya majawabu.
Mwandishi wa Nipashe Charles Mwakenja, akiuliza swali katika mkutano huo, Baraza lina mpango gani wa kupunguza hiyo adhabu waliotowa kwa Wanafunzi.
Mwalim Haji na Mwalim Hassan wakifuatilia makaratasi ya mitihani ya Watahiniwa wa kidatu cha Nne, yalioletwa na Katibu Mtendaji waBaraza la Mitihani ikiwa ni vielelezo kuonesha hakuna Mwanafunzi alioonewa katika adhabu hiyo.
Viongozi wa Chama cha Walimu Zanzibar , wakiangalia moja ya karatasi za mitihani ambazo zimekutwa na makosa na kufutiwa watahiniwa wake, wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya bwawani.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Dk Joyce Ndalichoka, akitowa maelezo ya kufutiwa mitihani watahiniwa wa kidatu cha Nne, wa mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment