Mvua kubwa iliyonyesha Desemba 18, mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika mtaa wa Ikuti Kata ya Iyunga, wilaya ya Mbeya, imebomoa zaidi ya nyumba 30, hali iliyopelekea wananchi zaidi ya 100 kukosa mahali pakuishi na msaada wa haraka wa vyakula na madawa unahitajika ili kuweza kunusuru maafa. Mbali na nyumba kubomoka mvua hiyo iliyodumu kwa muda wa masaa mawili imeweza kuharibu mimea ya mazao shambani. miundombinu ua Maji, Umeme na Barabara kutokana na mafuriko.
Vitongoji vilivyoathiriwa na mvua hiyo katika kata hiyo ni pamoja na kitongoji cha Inyala, Ikuti na Maendeleo.
Chanzo: BOFYA
0 comments:
Post a Comment