Makaburi
Shule Ya Msingi Veta
************
Mgogoro mkubwa umeibuka baina ya halmashauri ya Jiji la Mbeya na mmiliki wa makaburi 36 mzee Amilikiye Mwakibete Mkazi wa Kata ya Mwakibete baada ya uongozi kutaka kuyaondoa ili kupisha upanuzi wa eneo la shule.
Makaburi hayo ambayo yapo jirani na shule ya msingi Veta kata ya Mwakibete jijini Mbeya yanatakiwa kuondolewa ili kupisha upanuzi wa wa eneo la shule lifike hekta 1.5 kama sheria ya ujenzi wa shule inavyosema.
Imeelezwa kuwa mzee Mwakibete anakataa kwa madai kuwa yeye ndiye muasisi wa eneo hilo na ndiyo maana likapewa jina lake hivyo hawezi kuhama yeye wala kuhamisha makaburi hayo.
Kwa mujibu wa ofisa mipango Miji wa halmashauri ya jiji la Mbeya Efraim Mkumbo mgogoro alisema kuwa mara kadhaa mzee huyo amefuatwa kwaajili ya suala hilo lakini amekuwa akikataa na kusisitiza kuwa hatoweza kuyahamisha na badala yake amekuwa akiomba amilikishwe kisheria eneo hilo.
Alisema, mzee huyo alituma maombi ya kuomba kumilikishwa makaburi yaliyopo kwenye eneo la shule,barabara na eneo la wazi lililopo jirani na shule ambapoombi hilo lilifikishwa kwenye idara husika kwa ajili ya kujadiliwa.
Alisema, ombi lake baada ya kujadiliwa na halmashauri kupitia kikao cha kamati ya Mipangomiji na Mazingira cha agost 6 mwaka huu likakataliwa.
Alisema kuwa kikao hicho kiliazimia alipwe fidia ili aweze kuhamisha makaburi yake kutoka katika eneo la shule na kuyapeleka kwenye eneo rasmi la maziko aliki alipoarifiwa kwa barua hakukubaliana na mamuzi hayo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye hivi karibuni alitembelea eneo hilo aliuagiza uongozi wa halmashauri kupitia Meya Athanas Kapunga kutumia busara kuongea na mzee huyo ili wamweleweshe umuhimu wa kuhamisha makaburi hayo na si kutumia nguvu.
Chanzo: mbeyayetu.blog
0 comments:
Post a Comment