SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, November 8, 2011

Waziri Wa Zanzibar Bi Fatma Abdulhabib Akutana na Wazanzibar Waishio Miji Ya Delaware na Philadelphia Nchini Marekani

Waziri Fatma Fereji akipata picha ya pamoja na kina Dada waliofika kujumuika nae
 Mheshimwia Waziri Fatma Fereji ( wa pili kulia) akifurahia (akibeba) watoto wa kizanzibari waishio Marekani ama vizazi Vipya au Mabalozi Wapya wa Kuiwakilisha Zanzibar nje ya nchi. Katikati ni Engineer Salum Masoud (Mumu)
Waziri Fatma Fereji na Ofisa Suleiman (Personal Secretary wa Balozi) wa pili kulii pamoja na Said Mohammed Said wa kwanza kulia Wakifurahia machopochopo alioandaliwa na wageni wake wakiwa pamoja na Viongozi wa Zanzibar Diaspora Kulia Ustaadh Omar Ali.
 Baadhi ya akinadada waliokuwepo Delaware wakipata picha ya kumbukumbu na Waziri Fatma Fereji
 Dr Mohammed Adam akimtambulisha Waziri Fatma Fereji kwa Wazanzibari na kuwaeleza Wazanzibari umuhimu wa Diaspora kwa faida yao na nchi yao kwa ujumla manufaa yake
 Waalikwa pamoja na wenyeji wakiwa katika picha ya pamoja
Wawakilishi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ pia walikuwepo kutangaza juu ya utaratibu wa kutuma pesa bure nyumbani ukiweza kufungua Account yako Kwenye PBZ.Wa pili kushoto ni Katibu wa Zanzibar Diaspora Shamis Abdullaa na wa kwanza kushoto Juma Amour ( Managing Director of Peoples Bank of Zanzbar.)Picha Zote na Shamis Abdullah
---
Wazanzibari wanaoishi Miji wa Delaware na Philadelphia masaa Mawili kutoka Washington DC - Marekani kwa ushirikiano na Zanzibar Diaspora waliandaa tafrija hii  na kuweza kuwaalika Waziri Bi Fatma Abdulhabib Ferej pamoja ujumbe kutoka Zanzibar
Waziri Fatma aliwashukuru Wazanzibari Wanaoishi katika miji ya Delaware na Philadelphia na kuwapa ujumbe kuwa huu ndio Mwanzo wa mshikamano wa Wazanzibari aliowaagiza Makamo wa Pili wa Rais , Balozi Seif Iddi na kuwataka kila Mzanzibari alieko nje kuwa Balozi wa nchi yake kuitangaza Zanzibar.

Balozi Seif Aliwataka wazanzibari popote Duniani walipo waungane watafute maendeleo yao na bila ya kusahau nchi yao Zanzibar . 

Mwenyekiti wa Diaspora ya Marekani, Ustaadh Omar Ali na Katibu wake, Shamis Abdulla pia walijumuika na Wazanzibari kwenye Sherehe hii kuwakaribisha viongozi hao pamoja na Dr Mohammed Adam na Dr Talib Ali na Engineer Salum Masoud.

0 comments:

Post a Comment