SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, November 8, 2011

Prince Charles na Mkewe Camilla Duchess of Conrnwall Watua Zanzibar Kwa Ziara Ya Kutwa Moja

 Mtoto wa Malkia Elizabeth 11 Prince Charles akiwa na mkewe Duchess of Conrnwall wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ziara ya kutwa moja.
 Prince Charles akiwa na mkewe Duchess of Conrnwall waliovaa mashada ya mauwa wakipokelewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd mwenye suti nyeusi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ziara ya kutwa moja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akizungumza  na mgeni wake Prince Charless baada ya kumtembelea ofisini kwake Ikulu Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Moh’d Shein akibadilishana mawazo na wageni wake Prince Charles akiwa na mkewe Duchess of Conrnwall, kushotoni kwake ni Mke wa Rais Shein Mama Mwanamwema Shein hapo Ofsini kwake Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakitoa zawadi kwa Mtoto wa Malkia Elizabath 11 Prince charless pamoja na mkewe Duchess of Conrnwall hapo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Moh’d Shein Mwenye suti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake Prince Charles Ikulu Mjini Zanzibar.
Mke wa Prince Charles akiwa ameshikilia Mkoba wa Ukili ambao umetengenezwa na wajasiriamali wa Zanzibar baada ya kuwatembelea na kuangalia kazi zao,wa Mwanzo kulia ni Waziri wa Biashara Viwanada na Masoko Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui.
Prince Charles na Mkewe wakikabidhi msaada wa Vyandarua kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Saleh Ahmed Jidawi mwenye Shati Jeupe.
Prince Charles akisakata ngoma ya Uringe pamoja na Waziri wa Biashara Viwanada na Masoko Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui mwenye suti nyeusi katika Viwanja vya Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
Picha Zote na Yussuf Sima-MAELEZO-Zanzibar

0 comments:

Post a Comment