SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 25, 2011

Watu wasiopungua 200 wafariki dunia katika tetemeko la ardhi Uturuki

Watu wasiopungua 200 wamefariki dunia nchini Uturuki baada ya kutokea tetemeko la ardhi mashariki mwa nchi hiyo. 
Tetemeko hilo la ardhi lililokuwa na ukubwa wa 7.2 kwa kipimo cha rishta, limeutikisha vibaya mji wa Van ulioko mashariki mwa nchi hiyo na kubomoa majengo mengi huku idadi kubwa ya watu wakisadikiwa kufunikwa na vifusi. 
Idris Naim, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki amesema kuwa, hadi sasa watu 200 wamethibitishwa kupoteza maisha yao kufuatia janga hilo la tetemeko la ardhi na kwamba wengine 1,000 wamejeruhiwa. Juhudi za uokoaji zinaendelea huku kukiwa na wasi wasi wa idadi ya waliopoteza maisha kupindukia 1,000.
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameutembelea mji wa Van uliokumbwa na tetemeko hilo la ardhi ambao unapakana na Iran na kusisitiza juu ya kuongezwa juhudi maradufu za uokoaji. 
Tetemeko la mwisho kubwa la ardhi kuikumba Uturuki lilikuwa lile la mwaka 1999 ambapo watu wapatao 20,000 waliuawa kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Na Salum Bendera

0 comments:

Post a Comment