Licha ya changamoto zinazowakabili wazee,timu ya wanaume nayo hawakuwa nyuma katika mbio za kukimbia na magunia.
Timu ya wanawake wakikimbia mbio za magunia katika kilele cha maadhimisho hayo.
aadhi
ya wazee toka mikoa mbalimbali nchini wakiandamana wakiwa wamebeba
mabango yenye ujumbe tofauti kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya
wazee duniani kitaifa yaliyofanyika mkoani Lindi.
Timu
ya wanaume nao hawakuwa nyuma kwenye mashindano ya kuvuta kamba.Wazee
hao wameiomba Serikali iwaingize kwenye mifumo ya mifuko ya afya kwa
kuchangiwa na halmashauri zao.
Wazee
wameipongeza serikali katika miaka 50 ya uhuru kuwatambua kama
rasilimali na hazina kubwa kutokana na uamuzi wake wa kutunga Sera ya
Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 pamoja na tamko lake la kutoa matibabu
bila malipo katika hospitali zote za Serikali.Pichani ni timu mojawapo
ya wazee toka mikoa mbalimbali wakivuta kamba kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya wazee duniani kitaifa mkoani Lindi.
Picha zote na Catherine Sungura-Mohsw.
0 comments:
Post a Comment