SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 3, 2011

Vodacom Tanzania Yadhamini Mashindano ya Uvuvi Kisiwani Sinda

Kikundi cha Sanaa cha Jambo brothers kutoka Zanzibar kikionyesha sarakasi mbalimbali katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyokuwa yakiendelea kisiwani humo, ambayo pia  yalidhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
Commodore Spiras Manoloudis wa Yatch Club jijni Dar es Salaam (kushoto) akitoa neon la shukrani kwa wadhamini wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda hivi karibuni ambao ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, (kulia) Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia) akimkabidhi zawadi  Alfred Charles kwa niaba ya timu yake baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa upande wa boti ya Mistress katika mashindano yaliyofanyika huko Sinda kisiwani mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Washindi wa  mashindano ya uvuvi ya Latham Open wakifurahia tuzo zao za ushindi mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika Kisiwani Sinda mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Mwanamuziki Mark Hart kutoka Afrika Kusini akitumbuiza katika mashindano ya uvuvi yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda mwishoni mwa wiki, mashindano hayo yaliyoshirikisha nchi sita yalidhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania. 
Wafanyakazi wa boti ya Mistress wakiwa wamebeba samaki zilizovuliwa katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi  yajulikanayo kama Latham Open yaliyoshirikisha nchi sita  na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania
Na H@ki Ngowi.

0 comments:

Post a Comment