Hapa
Mtoto Cecilia akitoka Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na
afisa mmoja wa Channel Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya
kwenda India.
Mtoto Cecilia wakati akiwaomba wasamaria wema waweze kumsaidia.
*********
Mtoto
Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari
akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza
kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo
lake kuvimba kama unavyoliona.
Taarifa
za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi .Hoyce
Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada
huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza
kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake
kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande
mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema
inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.
Kwa
hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie
dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake
sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze
kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona
hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapemakwa
uchunguzi tunaweza tukawahepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
Na H@ki Ngowi
0 comments:
Post a Comment