Abiria wakisubiri gari lingine ili waendelee na safari yao baada ya ajali kutokea.
Basi la Shabco Express ambalo lilikuwa likieleka Arusha leo limepata ajali baada ya kupinduka katika kona za Msambiazi, Korogwe.
Kwa mujibu wa abiria waliokuwa ndani ya basi hilo, walisema basi hilo lilipinduka baada ya kutaka kulikwepa gari dogo na kujikuta likitumbukia mtaloni kutokana na hali ya mvua na ukungu uliokuwa umeenea barabara nzima. Hakuna mtu aliyekufa katika ajali hiyo.
Gari hilo baada ya kupinduka.
Picha kwa hisani ya Kajunason Blog.
0 comments:
Post a Comment