Na.Catherine Sungura, Mbarali
Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,,ameipongeza zahanati ya uturo wilayani Mbarali kuwa ni ya mfano Tanzania kwa kuzuia vifo vitokanavyo na mama wajawazito na watoto wachanga
Waziri Ummy ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipoenda
kutembelea zahanati hiyo na kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa
kushirikiana katika kuzuia vifo hivyo.
“Ninawapongeza sana wananchi wote wa Uturo kwa kazi kubwa na
nzuri katika kudhibiti vifo vya watoto wachanga na akina mama,nataka
kuwathibitishia zahanati ya uturo ni ya mfano kitaifa.
Alisema haikubaliki kwa mwanamke yeyote Mjamzito kufariki kwa
sababu ya kutimiza haki yake ya kuzaliwa ya kuzaa,wanawake wameumbwa
kuzaa,hivyo hakuna mtu atakayeweka vikwazo mwanamke asizae
“Kila mwanamke anayebeba ujauzito, mategemeo yake yeye na
kichanga watakuwa hai na salama,hakuna mwanamke anayebeba ujauzito kwa
mategemeo ya mtoto wake kufariki”
Aidha,alisema anautambua mchango mkubwa kwa watoa huduma
ngazi ya jamii kwa kufuatilia wanawake wote wajawazito kuhudhuria
kliniki kipindi chote cha ujauzito pamoja n jamii yote kuwajibika na
kushiriki katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi
“Popote nitakapoenda na kusimama
kuzungumzia kupambana na vifo vitokanavyo na vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga,nitatolea mfano zahanati hii.
kuzungumzia kupambana na vifo vitokanavyo na vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga,nitatolea mfano zahanati hii.
Hata hivyo waziri Ummy alisema Moja ya kipaumbele chake katika wizara hii nikupunguza vifo vya mama wajawazito watoto wachanga
Katika pongezi hizo waziri wa afya,maendeleo ya
jamii,jinsia,wazee na watoto hakusita kuwapongeza wanaume wote kwa kuwa
jeshi la kupambana na vifo hivyo”wanaume wote wa vitongoji vya
ukwama,ukwishikiro,mtamba na ukwaviro asanteni sana ninyi ni wanaume
bomba kwa kuwajali wenza wenu na watoto.
Awali mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Wilison Chotamganga
alisema jitihada za kutokomeza vifo hivyo vilianza mwaka 1998 mara
alipohamishiwa kijijini hapo na kukuta matuta (makaburi)madogo mengi
hivyo akaamua kuunda uongozi wa watu watano kwa kila kitongoji na kuweka
mikakati ya kuzuia akina mama kujifungulia nyumbani na kila mwanaume na
mwenza wake wanahudhuria kliniki kuanzia ujauzito hadi mtoto
anapofikisha umri wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa takwimu za tanzania zinaonesha kila saa moja
mwanamke mmoja anafariki wakati wa kujifungua,hivyo kwa siku wanawake
ishirini na nne wanafariki,720 kwa mwezi na takribani wanawake 8,600
wanafariki kwa mwaka
0 comments:
Post a Comment