Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna
Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza
kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo
zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akiitazama Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita mara
baada ya kukabidhiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya
Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi ili fedha hizo
zikatumike kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt.
Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa
wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.
Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo
ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia
madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kabla ya kukabidhiwa hundi
kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza katika tukio hilo la upokeaji wa Taarifa yaUtendaji wa
TAKUKURU pamoja na upokeaji wa Hundi Kifani kutoka Taasisi ya Bunge
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo katika Hotuba yake ambayo pia alitengua uteuzi wa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Ane Kilango Malecela ambaye alikubali kutoa
taarifa ambazo si sahihi kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa,
japo katika uhakiki uliofanyika mara baada ya taarifa hiyo kumebainika
kuwa kuna zaidi ya watumishi 45 ambao ni hewa.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi
pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Utumishi na Utawala bora
Angela Kairuki Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John
Kijazi wapili kulia, Dkt. Tulia Ackson wakwaza kulia, Katibu wa Bunge
Dkt. Thomas Kashilillah wakwanza kushoto, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,
Kamishna Valentino Mlowola Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Taarifa ya
Mwaka ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi wa juu wa
Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa JKT wakisikiliza kwa
makini maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli aliyokuwa akiyatoa Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA
IKULU
0 comments:
Post a Comment