Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Annastazia Wambura akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
Bi Nahya Mansour alipowasili katika Ofisi za Wilaya hiyo kwa ziara ya
kikazi ya kukagua Viwanja vya makazi vya Shirika la Utangazi Tanzania
(TBC) vilivyopo wilayani humo.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Annastazia Wambura akizungumza na viongozi wa Wilaya ya
Kisarawe(Hawapo pichani) alipofika katika ofisi za Wilaya hiyo kwa ajili
ya ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Annastazia Wambura akipokea taarifa ya kiwanja cha Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) kilichopo eneo la Kimani katika Wilaya ya
Kisarawe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bi Mwanamvua Mrin
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Annastazia Wambura akitoa maelekezo kwa Meneja Miradi wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Mackselin Chota.
…………
…………
Na Shamimu Nyaki, WHUSM
Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura amemuagiza
Meneja wa Miradi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC ) Bw. Mackselin
Chota kuhakikisha kiwanja Na.1 Kitalu “B” kilichopo eneo la Kimani
wilaya ya Kisarawe kinapatiwa Hati Miliki ili kuepusha kuvamiwa pamoja
na migogoro inayoweza kutokea.
Agizo hilo amelitoa jumamosi
wakati alipotembelea kiwanja hicho na kueleza kuwa kiwanja hicho ni
lazima kiendelezwe kwa ajili ya kuwasaidia wafanyakazi wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo kiwanja hicho kilitafutwa kwa dhumuni
hilo.
“Naishukuru Halmashauri kwa
kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo,hivyo natoa siku saba kwa
idara ya Miradi ya TBC kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha kiwanja
hicho kinapatiwa Hati”.Alisema Mhe.Annastazia.
Aidha amewataka kuwasilisha
gharama zilizotumika katika ujenzi wa nyumba zilizopo katika eneo hilo
na wapi zimetoka na sababu zilizosababisha ujenzi huo kukwama kwa zaidi
ya miaka mitatu.
Akitoa maelezo kuhusu Kiwanja
hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi
Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa kiwanja hicho kilipimwa na ramani yake
ya upimaji ilipata kibali cha Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara
ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kusajiliwa kwa namba
68480,ramani namba E 292/83 ya tarehe 22 februari, 2012.
“Taratibu za umilikishwaji
zilifanyika kwa kuandaliwa gharama za kulipia kabla hati
haijaandaliwa,malipo hayo yalifanywa na TBC kupitia NMB na kuwasilisha
fomu ya malipo hayo(Bank pay in slip)”.Alisema Bi Mwanamvua.
Naye Meneja wa Miradi wa
Shirika la Utangazaji Tanzania Bw.Mackselin Chota amesema kuwa Shirika
hilo lina jumla ya viwanja 55 nchi nzima,ambavyo 19 kati ya hivyo vina
Hati miliki ambapo katika mkoa wa Pwani kuna kiwanja kimoja, Dar es
Salaam viwanja vitano ambavyo viko Pugu Road,Kunduchi, na TAZARA,
Mikocheni na Sinza.
0 comments:
Post a Comment