Akidai kwamba wachezaji wengi hawatambui ni jambo la fahari kuichezea nchi yako.
Ince alikuwa akizungumza katika matangazo ya BBC ya Radio 5 Live.
"Kuichezea England ilikuwa ni kufikia kilele cha
mchezo wako. Sasa sio muhimu sana kwa kuwa kuna ligi ya klabu bingwa na
ligi kuu ya Premier", alifafanua Ince.
Matamshi ya nahodha huyo wa zamani wa timu ya
taifa ya England ni kufuatia England kuponyoka kwa ushindi finyu wa 1-0
dhidi ya Wales katika uwanja wa Wembley, Jumanne iliyopita.
Ince, ambaye wakati mmoja aliichezea Manchester
United ya England, na vile vile Inter Milan ya Italia, anasema wachezaji
pia hutoa visingizio vingi wanapohitajika kuichezea timu ya taifa.
"Iwapo utaitwa kuiwakilisha nchi, ni lazima
uhakikishe upo. Siku hizi, kuna watu wanaotoa vijisababu - wamechoka, au
wamejeruhiwa - kwa sababu wanataka wawe katika hali nzuri ili waweze
kushiriki katika mechi ya mwishoni mwa wiki".
"Nilipoichezea England, kulikuwa na wachezaji
waliokuwa katika kikosi mwezi mzima, au katika kila mashindano, lakini
(kutokana na ligi ya klabu bingwa na Premier) sasa tuna wachezaji 40
wanaopata kuichezea nchi na wasiostahili. Inasikitisha", alielezea Ince.
Ince pia aliwalaumu mashabiki wa England kwa
kutoshangilia kikamilifu uwanjani wakati timu ilipocheza dhidi ya Wales,
na akasema anaamini timu ya England huwa na wasiwasi inapocheza
Wembley.
0 comments:
Post a Comment