Mv Spice ikiwa imezama pwani ya Nungwi.Picha kwa hisani ya Michuzi Blog.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa ni wenye huzuni sana wakati walifika eneo la tukio la ajali ya meli ya Spice Islander, iliyozama katika bahari ya Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi walionusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akifutana na msaidizi mkuu wa Kituo cha Afya kivunge,Tamim Hamadi, baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander, Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akiwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja,Nasra Muhsin,wa Ole Pemba akiwa amelazwa katika hopitali ya Kivunge kaskazini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa pili wa rais Zanzibar Balozi Idd Seif akishuhudia miili ya marehemu waliofariki katika ajali ya meli ya My Space Islander kisiwa cha Nungwi.
watoa huduma ya mwanzo wakiwa katika harakati za kuwasaidi wananchi waliokolewa katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander iliyozama jana katika Bahari ya Nungwi mkoa wa kaskazini unguja,meli hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Unguja kuelekea Pemba.
Askari wa vikosi nbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi waliookolewa katika meli iliyozama huko katika Bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja,wakifikishwa katika ufukwe wa Nungwi.
********************
Meli ya Spice Islander imezama usiku wa kuamkia leo ikiwa safarini kuelekea Pemba ikitokea bandari ya Malindi Unguja.
Meli hiyo inasemekana ilikuwa na abiria wapatao 610 ambapo juhudi za kuokoa majeruhi wa ajali hiyo zinaendelea hivi sasa.
Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu,
Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku.
Haji Ussi amesema meli hiyo iliondoka katika Bandari ya Malindi
Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata
hitilafu na kusababisha kubinuka na hatimaye kuzama kabisa.
Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,
lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.
Naibu Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya
usafiri vya binafsi kama boti ziendazo kasi vimekwenda eneo la tukio
kutoa msaada. Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helikopta yake kwenye
eneo la tukio.
Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa
meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo
ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda
kwenye tukio. Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na
wananchi wameombwa kuwa watulivu.
BLOG YAKO 24 SEVEN 365 INACHUKUA FURSA HII KUWAPA POLE WALE WOTE WALIOPOTELEWA NA KUFIWA NA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU KWA KUWA WASTAHIMILIVU NA KUWAPA MOYO.
"SISI WOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA"
MOLA AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU WOTE MAHALA PEMA PEPONI, AMIN.
0 comments:
Post a Comment