Anaitwa
Joseph Kashinye, Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Igunga.
"Ninashughulikia kupata mtandao wa uhakika. Leo siku haitoisha,
nitakuwa nimepata suluhu la tatizo la Mtandao. Nitawaporomoshea kila
kinachojiri huku. Asubuhi hii nimebahatisha kuingiza picha hiyo kwa
taabu, imenichukua saa mbili kuingiza picha moja! Pichani Kashindye
alikuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa Igunga katika uzinduzi wa kampeni
jana.
Mabango yenye ujumbe tofauti katika mkutano wa CHADEMA jana.
Katibu
mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa akihutubia mjini Igunga jana katika
uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni hapa.Dr Slaaa alisema CCM
hawana sababu ya kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ile kwani kwa kipindi
cha miaka 50 imeshindwa kumkomboa Mtanzania katika lindi la
umaskini.Aliongeza kuseam kuwa CCM wanachokizinatia ni kutumia kila
mbinu ili kushinda chaguzi na kushika dola ikiwa hawana malengo na
mikakati madhubuti ya kumkomboa Mtanzania. Aliwaasa wana Igunga
kumchagua Mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye, ili awe mwakilishi wao
kwani ni mtu makini anaetoka katika chama makini.
Mwenyekiti
wa CHADEMA,Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika
mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la igunga.Mbowe
alisema kuwa wana Igunga mungu amewapa bahati kubwa ya ufaya uchaguzi
muda ,fupi baada ya uchaguzi mkuu. Hivyo waitumie bahati hiyo wa
kufanya mabadiliko. CCM haistaili kurudishwa tena madarakani jimboi
hapa, kwani kuna masuala mengi ya msingi yanayohusiana na maendeleo ya
wananchi CC imeshindwa kuyatekeleza kwa kipindi cha miaka 50.
Ilifika
zamu ya Mgombea wa Ubunge jimboni hapa kwa Tiketi ya Chadema, Mwalimu,
Mkaguzi wa Elimu, Joseph Lashindye.Kashindye alisema kuwa wana Igunga
wtarajie mabadiliko ya haraka katika maendeleo.Yeye ameamua kwa
makusudi kuacha ualimu na kuingia katika ulingO wa siasa. Amefanya kama
Mwalimu Nyerere alivyofanya kwani Mwalimu Nyerere, aliaacha ualimu na
kujiunga na TANU, matokea ya uamuzi huo wa mwalimu hakuna Mtanzania
asiyeyaju.Na yeye alisema kuwa endapo wana-Igunga watamapa ridhaa ya
kuwa mwakilishi atasimamia kwa nguvu zake zote misingi ya utu,
uchapakazi na atahakikisha anaziba mianya yote ya rushwa katika
halmashauri ya wilaya, ili fedha zinazotafunwa na wajanja, zifanye kazi
iliyokusudiwa ya kuwaletea maendeleo wana- Igunga.
Mbunge
wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwahutubia wananchi wa jimbo la
Igunga jana jioni katikauzinduzi wa kampeni za ubunge jimboni humo.
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akiwahutumia wakazi wa Igunga.
Kutoka
kulia ni katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, Joseph Kashindye
mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga katikati na Mwenyekiti wa Chama hicho
na mbunge wa jimbo la Hai wakielekea kwenye mkutano.
Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika
mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la igunga.
Sehemu
Kubwa ya Umati wa Wanachama Wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema)akielekea kwneye uzinduzi rasmi wa kampeni za Kuwania
jimbo hilo.
Mabango yalikuwa ni mengi lakini pia jeshi la polisi lilihakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha.
Picha na Mdau Victor Makinda na CHADEMA
0 comments:
Post a Comment