Wamarekani huwenda wakaleta mageuzi ya uwongozi
Rais Barack Obama akiwahimiza wafuasi wake wajitokeze kwa wingi kupiga kura
Wapigaji kura wa Marekani wanashiriki katika uchaguzi wa kati kati ya mhula siku ya Jumanne, kuwachagua wabunge wa mabaraza mawili ya bunge ya serikali kuu pamoja na wajumbe wa serikali za majimbo na mitaa.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema mabadiliko yanaweza kuwa makubwa sana na kusababisha wa Democrats kupoteza udhibiti wa mabaraza ya Wawakilishi na Senet.
Kuna viti 30 vya barazala Senet vinavyogombaniwa kote nchini. Na wachambuzi wanasema mashindano yako makali sana katika majimbo ya Magharibi kama vile California, na kuweza kukipatia chama cha Republican wingi wa viti katika Senet.
Warepublicans wanahitaji viti kumi pekee kuchukua udhibiti wa Senet. Lakini uchunguzi wa mwisho wa maoni unaonesha hali inaweza kuwa ni ngumu.
Uwezekano wao wa kupata ushindi utakua katika baraza la Wawakilishi. Viti vyote 435 vya baraza hilo vinagombaniwa, na wachambuzi wanasema wa Republicans watapata viti 39 wanavyo hitaji kuchukua udhibiti wa baraza la Wawakilishi.
Wakichukua udhibiti huo itakua vigumu sana kwa Rais Barack Obama na chama cha Democratic kuendelea na ajenda yao ya kisiasa.
0 comments:
Post a Comment