Republican kulidhibiti baraza la wawakilishi
Rais Barack Obama.
WASHINGTON
Vyombo vya habari nchini Marekani vinabashiri chama cha Republican kitachukua udhibiti wa baraza la wawakilishi baada ya kupata ushindi katika viti kadhaa vya baraza hilo katika uchaguzi uliofanyika jana. Chama cha Republican pia kimechukua viti kadhaa katika baraza la Seneti. Kwa Republican kuchukua udhibiti wa baraza la wawakilishi ni pigo kubwa kwa chama cha Demokrat kinachoongozwa na Rais Barack Obama. Republican walichukua kiti cha kwanza katika baraza la seneti katika jimbo la Indiana na kushikilia kiti cha Kentucky. Jimbo la Arkansas pia sasa litawakilishwa na seneta kutoka chama cha Republican. Viti vyote 435 vya bunge la Marekani Congress vinagombaniwa huku kwa upande wa baraza la seneti kukiwa na viti 37 vinavyoshindaniwa- kutoka jumla ya viti 100. Kura za maoni zinaonyesha kuwa Wamarekani walikuwa wanaangalia hali mbaya ya uchumi walipokuwa wanapiga kura, huku wengi wakiwa hawajafurahishwa na matumizi makubwa katika serikali ya Rais Obama.
0 comments:
Post a Comment