SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, September 19, 2010

Ahmadinejad: Umoja wa Mataifa unapaswa kutoa fursa ya kiadilifu kwa mataifa yote


Sample Image
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa ujumbe wa taifa la Iran katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni amani na urafiki kwa mataifa yote. Rais Ahmadinejad ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili mjini New York Marekani atakakohudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Amewaambia waandishi habari katika uwanja wa ndege wa John F. Keneddy kwamba Iran inatarajia kwamba Umoja wa Mataifa utatekeleza vyema majukumu yake halisi na kuyapa mataifa mbalimbali fursa ya kiadilifu ya kushiriki katika kuendesha masuala ya dunia. Amesisitiza kwamba mataifa yote ya dunia yanapaswa kushirikishwa katika kuendesha masuala ya kimataifa na kuongeza kuwa uadilifu hauwezi kupatikana duniani bila ya kushirikishwa mataifa yote katika kusimamia masuala ya dunia. 
Katika siku saba za kuwepo kwake mjini New York, Rais Ahmadinejad atahutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kukutana na marais wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa vyombo vya habari vya kimataifa.

0 comments:

Post a Comment