Waziri wa michezo wa Afrika Kusini amesema,
aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nelson Mandela atahudhuria ufunguzi wa
sherehe za Kombe la Dunia.
Makhenkesi Stofile amesema Mandela mwenye sifa
ya kupinga ubaguzi wa rangi aliomba tiketi kwa ajili ya siku ya ufunguzi
na kufunga mashindano hayo.
Awali Mandela alisema alikuwa mdhaifu sana
kuhudhuria shindano hilo linaloanza wiki ijayo.
Bw Mandela atakayefikisha umri wa miaka 92 mwezi
ujao, alifanya kampeni ya kutaka Kombe la Dunia kufanyika Afrika
Kusini.
Bw Stofile amesema, "Mandela ametaka kuhudhuria
Kombe la Dunia."
Shirika lake la hisani, Mandela Foundation,
halijathibitisha kuhudhuria kwake, wakieleza kuwa ni kutokana na sababu
za kiusalama.
Takriban watu 350,000 wanatarajiwa kutembelea
Afrika Kusini kwa ajili ya Kombe la Dunia, ambapo inafanyika barani
Afrika kwa mara ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment