SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 3, 2010

Umoja wa Mataifa waitaka Israel iache mara moja kuizingira Ghaza

Sample ImageKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uache kuizingira Ghaza haraka iwezekanavyo.
Ban Ki-moon amesema hayo baada ya kurejea kutoka safari ndefu iliyompeleka hadi Brazil, Malawi na Uganda akisisitiza kuwa, tatizo kubwa lililopelekea kushuhudiwa shambulizi la utawala wa Kizayuni dhidi ya msafara wa meli za misaada siku ya Jumatatu, ni Israel kuendelea kuuzingira Ukanda wa Ghaza, kitendo ambacho amesema, si sahihi na hakikubaliki kabisa.
Itakumbukwa kuwa, siku ya Jumatatu, makomandoo wa jeshi la utawala wa Kizayuni waliuvamia kikatili msafara wa meli sita za misaada ya kibinaadamu ambazo ndani yake walikuwemo raia wa nchi 42 tofauti duniani na kupelekea zaidi ya watu 20 kuuawa na karibu 50 wengine kujeruhiwa. Jinai hizo za Wazayuni zimezusha maandamano na malalamiko makubwa kote ulimwenguni huku nchi kadhaa zikiwaita mabalozi wa Israel katika nchi hizo ili watoe maelezo kuhusu jinai hizo mpya za utawala wa Kizayuni.
Maandamano dhidi ya Wazayuni yanaendelea kushuhudiwa katika sehemu mbali mbali ulimwenguni.

0 comments:

Post a Comment