Washukiwa kumi wa uharamia raia
wa Somalia wanatarajiwa kuhamishwa kutoka Uholanzi na kufikishwa
mahakamani nchini Ujerumani.
Mahakama moja mjini Amsterdam iliidhinisha
washukiwa hao kuhamishiwa Ujerumani baada kukataa madai ya upande wa
utetezi ya kutaka washtakiwe nchini Uholanzi.
Washukiwa hao kumi walikamatwa kikosi maalum cha
wanamaji wa Uholanzi baada ya kushambulia meli ya mizigo ya Ujerumani
nje ya pwani ya Somalia mwezi April.
Waendesha mashtaka mjini Hamburg nchini
Ujerumani wanatarajiwa kuwashtaki washukiwa hao kwa kosa la utekaji
nyara.
Jaji katika mahakama ya Amsterdam aliamua kuwa
licha ya Uholanzi kuwa na mamlaka ya kuwashtaki washukiwa, hakuna sababu
za kutosha za kukataa kuwapeleka Ujerumani kushtakiwa.
Mawakili wa utetezi wamedai kuwa meli
iliyoshambuliwa ilikuwa na usajili wa Bahamas na wala si Ujerumani akama
ilivyodaiwa.
"Ikiwa tunaweza kuhakikisha kuwa hatujui meli
hiyo ilikuwa na bendera ya nchi gani, ikiwa tuna uhakika kuwa hakuna
nyaraka, nani mmiliki wa meli, kwa nini mahakama inasema hivyo
kiurahisi, inatosha, kuwa mnapaswa kwende Ujerumani?" wakili Michael
Balemans aliliambia shirika la habari la Reuters.
Meli ya MV Taipan ilitekwa nyara kiasi cha km
900 mashariki kwa pwani ya Somalia mapema mwezi April.
Manuari ya Uholanzi, iliyokuwa ikishika doria
kwenye maji ya Somalia ikiwa sehemu ya Muungano wa Ulaya ya kupambana na
uharamia, ilillazimika kuchukua hatua baada ya kupokea ishara ya hali
ya dharura.BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment