Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa jiwe la Msingi kuzindua rasmi stendi ya Mabasi mjini Mbinga Mkoani Ruvuma leo.Rais Kikwete yupo mkoani Ruvuma Katika ziara ya Kikazi kukagua miradi ya maendeleo.
Sehemu
ya Barabara ya Peramiho -Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78 iliyofunguliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine
wa Serikali wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga yenye
urefu wa Kilometa 78.
Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata
utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78Km huku
akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali na balozi wa China nchini.
Mamia
ya wakazi wa Mbinga wakifurahia wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli alipokuwa anamshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa Utendaji wake
mzuri wa kuwajali wakazi hao kwa kuwajengea miundombinu bora.
Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wa kwanza kulia
akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli kabla ya uzinduzi wa barabara
ya Peramiho-Mbinga 78km .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit
Mwambungu.
Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katikati
akimshukuru balozi wa China nchini aliye kushoto kwake kwa kazi nzuri
iliyofanywa na Mkandarasi kutoka China Kampuni ya Synohdro. Kushoto ni Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia pamoja na Mawaziri wengine waliohudhuria
ufunguzi wa barabara hiyo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa katika picha ya pamoja na
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na
Mawaziri waliohudhuria katika ufunguzi wa barabara ya Perahimo-Mbinga. Picha na Jackson Msangula
0 comments:
Post a Comment