SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, July 20, 2014

MEYA KINONDONI MH. YUSSUF MWENDA AFUTURISHA WANANCHI WA MANISPAA YAKE

Shehe wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda (mbele) akiowaongoza waumini katika swala ya Magharibi, kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kwa wananchi wa Manispaa yake, viongzoi wa kiserikali na kidini, Dar es Salaam jana. Kutoka kulia (mstari wa mbele) ni Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaabn Bin Simba, Imam wa Msikiti wa Alfarouq, Mwita Kambi, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, viongozi mbalimbali wa dini na wa kiserikali.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akiwaongoza wageni mbalimbali kupakua futari aliyoindaa kwa wananchi wa Manispaa yake, viongozi wa kiserikali na wa kidini, Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Shehe wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto0 akipata futari pamoja na Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba (kushoto kwake), Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Shehe wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda wakati wa futari aliyoiandaa kwa wananchi, viongozi wa kiserikali na kidini wa Manispaa yake, jijini jana.
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan (kulia) akibadilishana mawazo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa tatu kushoto) wakati wakipata futari iliyoandaliwa na Meya huyo kwa wananchi, viongozi wa kiserikali na kidini wa Manispaa yake, Dar es Salaam jana. Wengine ni Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba (wa tatu kulia), Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum (wa pili kulia) na viongozi wengine wa kidini na kiserikali.
Watoto kutoka votuo mbalimbali vya kulea yatima vilivyopo katika Manispaa ya Kinondoni wakipata futari iliyoandaliwa na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na wageni waalikwa baada ya kupata futari aliyoiandaa kwa wananchi, viongozi wa kiserikali na kidini katika Manispaa yake, Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum kulia) na Shehe wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda (kushoto).
Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba (kulia) akitoa neno la shukran kwa wageni waalikwa baada ya kupata futari iliyoandaliwa na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda (kulia kwake) kwa wanananchi wa Manispaa yake, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Shehe wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akikabidhi zawadi za vyakula kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha MALAIKA wakati alipowaalika kufuturu nao pamoja katika futari aliyoiandaa kwa wananchi wake wa Manispaa hiyo jana. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akikabidhi zawadi za vyakula kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha CHAKUWAMA wakati alipowaalika kufuturu nao pamoja katika futari aliyoiandaa kwa wananchi wake wa Manispaa hiyo jana. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki.

Meya wa Manipaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amewataka wananchi wa Manispaa yake na nchini kote kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza ili kupunguza tatizo la watoto wa mitaani na mayatima ambao wamekuwa wakiongezeka kila siku jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa futari aliyoiandaa kwa wananchi wa Manispaa yake, viongozi wa Kiserikali na kidini, Dar es Salaam juzi Meya huyo alisema kuwa Manispaa yake ni kubwa na hivyo endapo watu watachukua maamuzi ya kusaidia watoto hao basi tatizo hilo litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa katika Manispaa hiyo na jijini kwa ujumla.

“Wito wangu kwenu tuwasaidie watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu katika Manispaa yetu ili kuondoa tatizo hili la watoto wanaozagaa mitaani kwani nao wana haki kama walivyo watoto wengine wenye wazazi na wanaoishi kwenye mazingira mazuri. Nazungumza hili kwa kuwa hili ni tatizo sugu katika Manispaa yetu.” Alisema.

Aidha aliwahakikishia wananchi hao kuwa Manispaa itaendelea kufanya kila inachoweza kuhakikisha inaboresha hali ya maisha ya wananchi wake bila kujali itikadi za kisiasa wala kidini ili kuondoa umasikini kwa wananchi hao. Pia alisema Manispaa itaendelea kusimamia kampeni yake ya kuweka mazingira safi ya Manispaa kwa kuhakikisha inatimiza malengo yake iliyojiwekea.

“Niseme kuwa sisi (Manispaa) ndio tunaoondoa taka kwa asilimia 75 hapa jijini, nawapongeza Madiwani wangu kwa kusimamia vema kampeni mbalimbali tunazozianzisha katika Halmashauri yetu.” Alisema

Kwa upande wake Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Saluma aliwahimiza waumini wa dini ya Kiislam kuzidisha ibada katika kumi hili la mwisho la mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kusema kuwa endapo muumini atakutwa na usiku wa lailatul qadir basi ni sawa na kufunga miezi 1000 ambayo ni sawa na miaka 83.

0 comments:

Post a Comment