Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.
MTANDAO
wa Wanawake na Katiba umevitaka vyombo vya habari kuacha kuyumbushwa na
upepo wa kisiasa katika suala zima la kupigania mambo ya msingi kwa
jamii ambayo yanaitaji kuingizwa kwenye Katiba mpya kwenye mchakato
unaoendelea hivi sasa wa kuandika katiba mpya.
Kauli
hiyo imetolewa na baadhi ya wajumbe wanaounda mtandao huo jijini Dar es
Salaam walipokuwa wakizungumza na wahariri wa vyombo vya habari
kuelezea msimamo wa wajumbe hao kwenye mchakato wa uandikaji katiba
mpya.
Mwakilishi
kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu aliviomba
vyombo vya habari kuwaunga mkono wanamtandao hao ambao pamoja na mambo
mengine wamejipanga kupigania kero za wananchi kuhakikisha zinapata
majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya hivyo kuwataka wanahabari
kuwaunga mkono.
Alisema
vyombo vya habari visikubali kupelekeshwa na wanasiasa kwa kupaza sauti
kwenye maslahi ya wanasiasa zaidi na kushindwa kujadili masuala ya
msingi ya jamii, ambayo endapo yatapata majibu katika mchakato wa
uundaji katiba mpya wananufaika ni wananchi wote tofauti na masuala ya
utawala (madaraka).
“Waandishi
wa habari msikubali kuchezeshwa ngoma za wanasiasa, ambao mara zote
wanapigania maslahi yao kiutawala…tupiganie maslahi ya jamii, jamii
inaitaji kuona huduma bora za afya, elimu na mgawanyo sawa wa
rasilimali,” alisema Dk. Semakafu.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja
wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada kwa
wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari alisema vyombo vya habari vina
nguvu za kipekee katika kuleta mabadiliko kwenye jamii na mamlaka hivyo
kuwaomba watumie fursa hiyo ipasavyo katika kupigania maslahi ya umma.
“…Hivyo
vyombo vya habari, kama msingi wa kupatikana kwa taarifa yoyote, na
kuongoza katika ushawishi vina sehemu muhimu sana katika kuongoza kuleta
mabadiliko yawe ya sera, tabia au utamaduni,” alisema Bi. Msoka ambaye
pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba.
Hata
hivyo alivitaka vyombo vya habari kuwaunga mkono wanawake kwani licha
ya kuwa na mchango mkubwa katika jamii wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto nyingi zikiwemo za kusahaulika kwenye fursa anuai zilizopo.
“…Wanawake ni asilimia 80 ya nguvu kazi vijijini na ni asilimia 60 ya
wazalishaji wakuu wa chakula…lakini tunachangamoto nyingi,” alisema Bi.
Msoka.
Mtandao
wa Wanawake na Katiba ni muunganiko wa asasi za kijamii na kitaaluma
zipatazo hamsini zilizoungana kudai katiba inayozingatia masuala ya
kijinsia na inayotokana na mchakato ulioshirikisha sauti za makundi
yote.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
0 comments:
Post a Comment