MASHINDANO YA BAISKELI VODACOM - SHINYANGA BINGWA!
Washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge Kilometa 196 kwa wanaume wakichuana vikali katika mbio hizo zilizofanyika jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa kamati ya ufundi Taifa Godfrey Jax Mhagama akitoa maelezo kwa washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge kabla ya mbio hizo kuanza rasmi zilizofanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro, akiinua bendera kama ishara ya uzinduzi rasmi kwa mbio za Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa wanaume na wanawake.
Washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge Kilometa 196 kwa wanaume wakichuana vikali katika mbio hizo zilizofanyika jijini Mwanza.
Mshindi wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa upande wa wanaume Hamiss Clement(shinyanga) akimalizia mbio hizo na kuibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia Masaa 5:19:43,kwa kilometa 196.
MASHINDANO YA BAISKELI VODACOM - SHINYANGA BINGWA!
Mwandishi Wetu,.Mwanza
HAMISI Clement wa Shinyanga leo ( jana) alinyakua taji la’ Vodacom Mwanza Cycle Challenge’ lililokuwa likishikiliwa na Mussa Milao wa Arusha na kuzawadiwa sh mil 1.5 na waandaaji wa mashindano hayo baada ya kutumia saa 5:19.43.
Clement katika mashindano hayo alishiriki mbio za umbali wa Kilomita 196, abazo zilianzia Nata hadi Nyashimo ambako alitumia baiskeli ambayo si ya mashindano ambako liwaacha mbali wenzake wengi waliokuwa na baiskeli za mashindano.
Mshindi wa pili wa mashindano hayo kwa wanaume ni Richard Laizer aliyetumia saa 5:20.12 ambaye alizwadiwa sh mil 1 huku wa tatu Said Konda wa Shinyanga abaye alitumia saa 5:20.30 ambaye alizawadiwa sh 700,000.
Kwa upande wa Wanawake Sophia Adison wa Arusha naye alinyakua taji la mashindano hayo baada ya kushika nafasi ya kwanza ya mashindano hayo baada yakutumia saa 2:32.14 na kuzwadiwa sh mil 1.1, taji ambao lililuwa likishikiliwa na Beatrice Kennedy wa Dodoma ambaye mwaka huu amenyakua nafasi ya tano ya mashindano hayo.
Mshindi wa pili kwa wanawake ni Martha Anthony wa Mwanza ambaye alitumia saa 2:34.27 ambaye alizawadiwa sh 800,000 huku wa tatu alikuwa ni Ndyashimbi Kurya wa Mwanza alinyakua nafasi ya tatu baada ya kutumia saa 2:36.34.
Adison katika mashindano hayo alishiriki mbio za umbali wa Kilomita 80, kutokea Nata hadi Nyanguge ambako uzoefu ulimsaidia kunyakua taji hilo.
Akizungumza baada ya mashindano hayo, Clement alisema kilichomsadia ni mazoezi ya mara kwa mara aliyokuwa akiyafanya ingawa milima ilimsumbua katika mashindano hayo.
Clement alisema kwa ushindi huo atawashauri wenzake wa Shinyanga kununua baiskeli za mashindano kwa sababu, baiskeli za kawaida zinasumbua, fedha alizozipata atatumia kununulia baiskeli za mashindano.
Naye Adison alisema mashindano ya mwaka kwake yalikuwa na upinzani mkali kwa sababu ushindani ulikuwa ni wa hali ya juu hasa wenye baiskeli za Phoenix ambao walikuwa hawampi nafasi.
Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Steven Kingu alipongeza ushindi wa Clement kwa sababu mara nyingi ushindi huenda mikoa mingine ambako pia alitoa wito kwa washiriki wa mikoa ya Kanda ya ziwa kuwa na baiskeli za kisasa na za mashindano ili wafanye vizuri zaidi katika mashindano ya Kimataifa.
Kingu alisema mara zote Vodacom kila mwaka wanatoa zawadi zaidi ya mwaka uliopita ili kuleta chachu ya washiriki kujiandaa vilivyo kwa mashindano yajayo na kutoa wito kwa mashindano ya mwakani.
Mgeni rasmi katika mashinano hayo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Kanali Mstaafu Serenge Mrengo.
Mashindano hayo yalishirikisha washiriki 403 kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam, Dodoma, Mara na Kagera.
0 comments:
Post a Comment