|
Msafara wa gari chache majira ya saa 2:30
ulianza safari katika viwanja vya Usa-River ambako gari za maharusi
zilikuwa zikipambwa mdogo mdogo zikapanda Kilima zikiwa na maharusi
Joshua Nassari na Anande Nnko safari ilikuwa ni kanisa la Kipentekoste
la Kilinga,Meru tayari kwa ajili ya Ndoa. |
|
Hatimaye Bw Harusi Joshua Nassari anateremka
katika usafiri wake aina ya Range Rover muda mfupi baada ya kufika
katika viwanja vya kanisala la Kilinga maarufu kama kwa Mchungaji
Babu. |
|
Wageni mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ya
ndoa mmoja wapo ni huyu ,Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Job Ndugai(katikati) |
|
Bibi Harusi Anande Nnko alikuwa ni mwenye
furaha kila wakati ,"Full Tabasamu." |
|
Wenyeji katika shughuli hiyo akiwemo mzee
Samweli Nassari ,baba mzazi wa Jishu walikuwa wamevalia mavazi nadhifu
aina ya suti wakingojea ugeni uliokuwa ukiwasili katika kanisa la
Kilinga. |
|
Hataimaye Bw Harusi Joshua Nassari akaingia
kanisani yeye na wapambe wake na hapa anaye ngojewa ni Bibi Harusi
Anande Nko. |
|
Bi Harusi Anande Nko akashuka katika gari
alilokuja nalo aina ya Land Cruser VX. |
|
Bwaa Harusi Joshua Nassari akamvisha pete
mkewe Anande Nnko. |
|
Bibi Harusi Anande Nnko akamvisha pete
mumewe Joshua Nassari |
|
Kisha Maharusi
wakapongezana. |
|
Maharusi wa wakawekewa mikono na Maskofu
wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT)
David Batenzi. |
|
Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria
ibada hiyo (hawapo pichani) |
|
Maharusi wakionesha pete zao za ndoa muda
mfupi baada ya kuvishana. |
|
Uthibitsho wa ndoa ni vyeti vya ndoa ,na
hapa maharusi wakitia saini katika vyeti vyao. |
|
Wagebi mbalimbali walihudhuria ibada hiyo
,na hapa ni mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (wa
kwanza) |
|
"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa
vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti
vyao vya ndoa. |
|
Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei
na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo. |
|
Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi
Anande Nnko. |
|
Bw na Bi Joshua Nassari na wakiweka Sadaka
zao katika kapu la sadaka. |
|
Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na
Mzee Edwin Mtei. |
|
Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na
maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea
uwanjani. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii
kanda ya kaskazini.
|
Mbunge
Joshua Nassari na Anande Nnko wakiwa mbele ya zawadi yao ya
Ng'ombe ilitolewa na waumini wa Kanisa la Kilinga ambako ibada ya ndoa
ilifanyika,kanisa linaloongozwa na Mchungaji Babu.
|
|
Mbunge
Joshua Nassari na Anande Nnko wakiteta jambo .
|
|
Baba Mzazi wa Joshua Nassari,Mzee Samwel
Nassari akimpongeza mwanae kwa hata hiyo. |
|
Mamsapu akianza majukumu ya kuhakikisha Mzee
anakuwa nadhifu kila wakati. |
|
Maharusi wakaaga katika viwanja vya Kanisa
la Kilenga . |
|
Bi Harusi Anande Nnko akiwa katika gari
tayari kuelekea katika viwanja vya Usa-River Academy. |
|
Mbunge
wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari na ,Anande Nnko
wakiwa ndani ya gari muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la
Kilinga wilayani Arumeru tayari kwa kuelekea viwanja vya Usa-River
Academy.
|
|
Msafara ukaanza safari ya kuelekea barabara
kuu ya Moshi/Arusha ukitokea kanisani Kilinga. |
|
Baadae maharusi wakabadili gari ili waweze
kuonekana vyema na wakazi wa jimbo la Arumeru
Mashariki. |
|
Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku
wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani. |
|
Mharusi waki "Show Love" |
|
Kila sehemu msafara wa magari ya maharusi
ulipopita ,wakazi wa maeneo hayo walionesha furaha zao
. |
|
Barabarani kulijaa watu wakimshangilia Mbune
wao akijinyakulia Jiko. |
|
Kama kawaida Jasiri haachi
asili na muacha asili ni hasidi na hana akili. |
|
Msafara wa magari ulikuwa ni mrefu
. |
|
Madereva wa boda boda pia walikuwepo
kuongoza msafara . |
|
Wananchi hawa jamii ya Maasai walitembea
umbali mrefu na msafara huku wakiimba nymbo na hatimaye msafara
ukaingia Ngurdoto Mountain Lodge kwa ajili ya upigaji wa picha
. |
Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda
ya kaskazini alikuwa katika sherehe hiyo matukio mbalimbali mtaendelea
kuyapata hapa na http://dixonbusagaga.blogspot.com.