Waziri
wa Maji Professor Jumanne Maghembe (kulia) akikagua bidhaa za mabomba
yanayozalishwa na kiwanda cha Pipe Industries cha mjini Dar es salaam
wakati wa kongamano la wataaalam wa maji lilifanyika hivi karibuni. wa
pili kushoto ni Mwekezaji Mzawa wa Kiwanda hicho Bwana Nassor Ally Seif.
Mwekezaji
Mzawa wa Kiwanda cha Pipe Industries Bwana Nassor Seif (kushoto)
akimsikiliza Waziri wa Maji Professor Jumanne Maghembe akimweleza jambo
kuhusiana na mabomba yanayozalishwa na pipe industries wakati akikagua
maonyesho ya kiwanda hicho katika kongamano la maji lilofanyika mjini
dar es salaam.
Waziri Mageembe akizungumza na waandishi wa habari baaada ya kufungua kongamano la maji.
Waziri
wa Maji Professor Jumanne Maghembe (wa pili kutoka kushosto) akifurahia
jambo na wamiliki wa pipe industries bwana nassor seif (kushoto) na
seif seif (wa pili kulia) wakiwa na baadhi ya washiriki wa kongamano la
maji. kulia ni bibi esther baruti kroll mwakilishi mkazi wa kampuni ya
saruji ya dangote industries.
wataalam
vijana wa tanzania ni miongoni mwa washiriki na wawezeshaji wa
kongamano la maji. kushoto ni moses nkanda bingwa katika mambo ya
mabomba ya gesi na mtaalam mshauri bwana subiro mwapinga.
Mtoa
Mada katika Kongamano la Teknolojia ya Maji kutoka Kampuni ya
Borouge,Bwana Mario Andrade akitoa maelezo kwa washiriki wa kongamano la
maji juu ya borouge na uwezo wake katikasekta ya mabomba.
washiriki wakifuatilia kongamano.
Mkurugenzi wa Superdoll,Bwana Jamal Bayser (kulia) na Mkurugenzi wa Reni International,Bwana Dipak Vassa.
Meneja
wa Mradi wa Kiwanda cha Mabomba cha Pipe Industries,Bwana Sebastian
Kyoni (kulia) akiwa na wataalam wenzake wakishiriki katika kongamano la
maji jijini dar es salaam.
waziri wa maji professor jumanne maghembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano la maji.
meneja
wa super star forwarders bwana fulgence bube (wa pili kulia) akielezea
jambo kwa washiriki wenzake wa kongamano la maji. wa pili kushoto ni
mkurugenzi wa superdoll bwana jamal bayser.
Bwana
Andrew Wedgner wa Kampuni ya Borouge ya falme za kiarabu akitoa utalaam
wake juu ya mabomba ya pe 100 wakayi wa kongamano la maji lilokuwa
linafanyika mjini dar es salaam. kushoto ni bwana reda ashkar ambaye
amebobea katika uunganishaji wa mabomba ya hdpe na ufundishaji wa
teknolojia hiyo btoka kampuni ya borouge.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Pipe Industries Bwana Seif Ally Seif akitoa maelezo ya
kiwanda chake katika kongamano la maji lilofanyika jijini dar es salaam.
======
Wiki
hii jijini Dar es salaam kumefanyika Kongamano kubwa la wadau wa maji
kutoka kila kona ya nchi hii. kubwa lililofanyiwa kazi na wataalam hao
wa maji ni kujulishwa teknolojia mpya ya mabomba iliyokuwa
inatambulishwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya mambomba ya Borouge
kutoka Falme za Kiarabu.
Borouge
ilileta wataalam wanne ambao ni Mario Andrade, Farraj Tashman, Andrew
Wedgner na Reda Ashkar. walionufaika na mafunzo hayo ni waliotoka
Mamlaka za Maji mijini na vijiji, Wahandisi, Washauri katika fani zote
za maji, ujenzi na gesi.
pia
washiriki walifahamishwa kuwa sasa lile tatizo la mabomba ya matumizi
yote yamefika mwisho kwani kiwanda cha pipe industries cha vingunguti
mjini dar es salaam kitakidhi mahitaji ya nchi nzima na kuwa na ziada ya
kuuza nje kwa amabomba ya aina zote kama vile hdpe, pvc, grp na mabomba
chuma kwa upenyo wa 60mm mpaka zaidi ya 3,200mm.
Mgeni
Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Waziri wa Maji,Professor Jumanne
Maghembe ambaye alionyeshwa kufurahishwa kwake na uwepo wa kiwanda kama
hicho ambacho kinamilikiwa na wazawa kinahesabika kama kikubwa kuliko
vyote afrika mashariki na kati pia cha aina yake kwa kuweza kuwa na
uzalishaji wa mabomba aina yote katika kiwanda kimoja na chenye uwezo wa
kuajiri watu 500.