Wafanyakazi
wa duka jipya la Tigo la Lindi Mjini katika nyuso za furaha na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (aliyebeba
mfuko wa Tigo) wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya iliyofanyika
juzi.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (kushoto) akimsikiliza
kwa makini Meneja wa duka jipya la Tigo lilipo Lindi Mjini Bw. Ahadi
Mtweve (katikati) kuhusu huduma ya mauzo ya simu za kisasa pale
alipofika kuzindua duka hilo juzi. Duka hilo linalopatikana mtaa wa
Makongoro nyuma ya stendi kuu ni duka la 41 la Tigo nchi nzima.
Meneja
wa duka jipya la Tigo lililopo Lindi Mjini Bw. Ahadi Mtweve (katikati)
akimuelezea Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda
kuhusu huduma ya Tigo Pesa inayopatikana kwenye duka hilo mpya
liliozinduliwa juzi na Mkurugenzi huyo. Kushoto ni mtoa huduma wa Tigo
Pesa katika duka hilo Bi. Nasra Mbise. Duka hilo linalopatikana mtaa wa
Makongoro nyuma ya stendi kuu ni duka la 41 la Tigo nchi nzima.
Afisa
wa Mahusiano kwa Wateja wa Tigo Bi. Pilila Kavishe (kushoto) na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (wapili kulia)
katika picha ya pamoja na wateja wa Tigo waliozawadiwa kadi za
vipaumbele kutoka kampuni hiyo ya simu. Kazi hizo zinampa uwezo mteja wa
Tigo kupatiwa huduma za kipekee kama kutokukaa katika foleni anapofika
katika duka la Tigo pamoja na kuondelewa kwa gharama mbali mbali
anapohudumiwa katika maduka hayo.
Tigo
imefungua duka jipya la huduma kwa wateja mjini Lindi ambayo
itarahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa wateja wa mjini hapo ambao
awali walikuwa hawana namna ya kupata huduma za moja kwa moja kutoka
kwenye kampuni hiyo ya simu.
Uzinduzi
huo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi mjini, Kelvin
Makonda, ambaye ameipongeza Tigo kwa hatua yake ya kuzidi kusogeza
karibu huduma zake kwa watu wa Lindi.
“Pamoja
na utatuzi wa kero za mawasiliano naamini ya kwamba duka hili jipya
litakuwa kama kituo cha kutoa huduma mbali mbali ambazo wateja wenu wa
Lindi watakuwa wanahitaji kutoka kwenu kila siku,” alisema Makonda.
Makonda
alisema kwamba huduma mbalimbali za mawasiliano zitolewazo na kampuni
ya simu ya Tigo kama vile kupiga simu, kutuma SMS, mtandao wa Intaneti
pamoja na huduma ya kutuma na kupokea fedha, zimekuwa kichocheo kikubwa
katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. “Aidha huduma
hizi zimeleta mageuzi chanya katika ufanyaji biashara na kuinua hali ya
maisha ya maelfu ya wakazi wa Lindi na mamilioni ya watanzania kwa
ujumla,” alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Tigo wa kanda ya Pwani Bw. Brian Kalokola,
amesema tawi hilo ambalo linalopatikana Lindi mjini mtaa wa Makongoro
karibia na stendi kuu linatarajia kuwahudumia wateja wapatao 150 kwa
siku kwa kuwapa huduma mbali mbali za Tigo zikiwemo huduma ya
kuunganishiwa intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma
maalum za simu za kisasa (“Smartphones”).
“Duka
hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu limeleta huduma zetu
karibu zaidi kwao. Pia linapatikana sehemu nzuri kibiashara kiasi kwamba
litavutia hata wateja kutoka wilaya zingine na maeneo jirani kama
Nachingwea, Liwale, Kilwa, Ruangwa na Lindi vijijini,” alisema Kalokola.
Duka
hili linatoa huduma nyingine maalum zikiwemo uuzaji wa bidhaa mbali
mbali kama simu za kisasa ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribisha kabla
ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi katika
kuchagua na kununua bidhaa inayokidhi mahitaji yake.”
Tawi
la Lindi linafikisha jumla ya maduka yanayoendeshwa na kampuni ya Tigo
nchini kufikia 41. Kwa mujibu wa Kalokola, kampuni hiyo ina mipango ya
kufungua maduka mengine mengi zaidi katika sehemu mbali mbali nchini.