Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wasioona Malangali Mwl. Orthor M. Mkangara
akitoa maelezo mafupi ya shule hiyo iliyoanzishwa rasmi mwaka 1998
ambapo mpaka hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 71 wengi wao wakiwa
wasioona na baadhi wakiwa ni walemavu wa ngozi "Albinism". Alisema kwa
sasa shule hiyo inahitajio kubwa na vifaa vya kufundishia pamoja na
usafiri kwa ajili ya kurahisisha shughuli mbalimbali shuleni hapo.
Alisema kuwa zipo changamoto nyingi shuleni hapo ambapo wadau mbalimbali
wanakaribishwa katika kusaidia kuzitatua. Aliwashukuru kikundi cha
kinamama kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa (pichani kushoto) kwa msaada
waliotoa na kuomba wadau wengine kuwa na moyo kama huo katika kusaidia
watoto wenye ulemavu hapa nchini.
Katibu
wa Kikundi cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. Joyce
Mwanandenje akizungumza kwa niaba ya umoja huo ambapo alisema lengo la
ujio wao Shuleni hapo ni kutimiza desturi yao ya kila mwaka ambapo
hutembelea makundi ya wahitaji mbalimbali katika kuadhimisha siku ya
wanawake duniani. Katika salam zao shuleni hapo walitoa msaada wa
magodoro 20, Sukari, sabubi na zawadi mbalimbali kwa aijili ya
wanafunzi. Kikundi hicho cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
kinaundwa na watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hazina
Ndogo, Ukaguzi wa Ndani, Chuo Kikuu Huria na Baraza la Nyumba na Ardhi
Mkoa.
Baadhi
ya wanafunzi shuleni hapo wakiimba wimbo mwanana wa kuwakaribisha
kikundi cha kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa walipofika shuleni
hapo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. S. Mwasilu akimkabidhi Mkuu wa Shule ya
Msingi Wasioona ya Malangali Mwl. Orthor M. Mkangara msaada wa magodoro
na zawadi mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.Mwenyekiti
wa Kikundi cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. S. Mwasilu na
Katibu wake Bi. Joyce Mwanandenje wakigawa zawadi za biskuti kwa
wanafunzi wasioona wa Shule ya Msingi Malangali katika hafla fupi ya
kutoa msaada shuleni hapo.
Sehemu ya Msaada uliotolewa shuleni hapo.
Msafara wa kikundi cha kinamama wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakiingia kuangalia mabweni shuleni hapo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wasioona Malangali Mwl. Orthor M. Mkangara
akitoa maelezo mafupi kwa kikundi hicho cha kinamama walipoingia kukagua
mabweni shuleni hapo, Mwalimu huyo alishukuru kwa msaada walioutoa wa
magodoro na kusema utasaidia sana kuondoa tatizo la upungufu wa magodoro
uliokuwepo.
Hakika
msafa huu wa kikundi cha kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ulikua
na mengi ya kujifunza shuleni hapo. Uandishi na namna ya kusoma kwa
watu wasioona ni tofauti kabisa na uandishi wa kawaida. Hutumia kifaa
maalum kuandikia, kalamu maalum na karatasi maalum, hali kadhalika
usomaji wa maandishi hayo huwa ni wa kupapasa.
Wanafunzi
wasioona hutumia kifaa maalum kwa ajili kuandikia maandishi yenye nundu
ambayo husomeka kwa njia ya kupapasa. Kalamu ya kuandikia huwa na ncha
kali kama sindano ya fundi viatu. Karatasi za kuandikia huwa ngumu
kuweza kutoa vinundu ambavyo husomeka kwa kupapaswa.
Mwanafunzi
S. Ngajiro ambae alikuwa haoni kabisa alipojiunga shuleni hapo na
kubahatika kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Dar es
Salaam na kufanikiwa kuona akitumia mashine maalum ya kuandikia ("Tyre
Writter") kwa ajili wanafunzi wasioona shuleni hapo. Mashine hiyo maalum
kwa ajili ya watu wasioona ina vitufe sita tu vya kuandikia ambavyo
hutumika kutengeneza Alfabeti zote katika uandishi wa lugha kwa kutumia
ujuzi wa hali ya juu.
Moja ya darasa dogo kabisa shuleni hapo ambalo huchukua wanafunzi wasiozidi tisa.
Kikundi
cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakiangalia bustani ya
mbogamboga ambayo ina hudumiwa na wanafunzi shuleni hapo.
Picha
ya Pamoja kati ya uongozi wa shule ya wasioona Malangali, kikundi cha
kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa na baadhi ya wanafunzi wa shule
hiyo.
Picha na Habari na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com