Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu Chungu na Vibuyu, vilivyotumika kuchanganya Udongo
wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964, kutoka kwa Mawazo Ramadhan wa Makumbusho
ya Taifa, wakati alipotembelea kwenye Banda la Idara ya Muungano Ofisi ya
Makamu wa Rais, alipotembelea maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50
ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa na Ofisa wa Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha
Mashuki, baadhi ya Magazeti yaliyochapishwa
mwaka 1964, wakati alipotembelea kwenye Banda la Idara ya Muungano Ofisi ya
Makamu wa Rais, alipotembelea maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50
ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata
maelezo kuhusu shughuli za Bunge kutoka kwa Ofisa Habari wa Bunge, Prosper
Minja, wakati alipotembelea kwenye Banda hilo, kwenye
maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea
kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, apata
maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Magishi Mgasa, alipokuwa
akitembelea kwenye Mabanda ya maonyesho
ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.