Padri atishia kuchoma Qurani
Padre Terry Jones.
Padri wa kanisa la kiinjili na wafuasi wake, kuadhimisha kumkumbu ya Septemba 11, kwa kuzichoma Quruani.Maafisa
wa utawala wanasema padri huyo wa Florida na wafuasi wake wana haki ya
kikatiba kuchoma Quraani, kama walivyofanya hapo zamani waandamanaji
waliopinga vita hapa Marekani walipochoma bendera ya Marekani kwenye
maandamano.
Lakini
wanasema wanamatumaini kuwa kanisa hilo litafikiria tena kuchukuwa
hatua hiyo, na kujaribu kutafuta njia nyingine ya kuadhimisha kumbukumbu
ya September 11 bila kuchukuwa hatua ambazo zinaweza kuchochea
upinzani dhidi ya Marekani na kusababisha ghasia nje ya nchi.
Katika
ujumbe wa utawala uliokuwa na maneno makali, ulisema mipango ya padri
wa kanisa la kiinjili huko Florida, Terry Jones, haikubaliki, ni chuki
na haifai kufanyika, alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje, P.J
Crowley.
“Tunadhani
vitendo hivi ni vya uchokozi, havina heshima, havistahmiliki, vita
leta mgawanyiko na tunafahamu kuwa watu kadhaa wamejitokeza na kupinga
kile ambacho padri huyu na wafuasi wake wanataka kufanya. Tungependa
kuona wamarekani zaidi wanasimama kidete na kusema jambo hili halipo
katika thamini za kimarekani, kwa kweli ni hatua ambazo ni kinyume na
maadili ya kimarekani,” alisema Bw. Crowley.
Msemaji
huyo alisema kuwa ingawaje ni upinzani dhidi ya msimamo mkali wa
kidini, lakini kuchoma Quraani huenda kukachochea msimamo mkali zaidi.
Akielezea
onyo la kamanda wa vikosi vya Marekani huko Afghanistan jenerali David
Patreus, alisema hatua hiyo inaweza kutumiwa vibaya na kundi la Taliban
kueneza propaganda zao. Crowley anasema hiyo inaweza kuwa na athari
mbaya kama zilipotolewa picha za wanajeshi wa marekani wakiwaadhibu
wafungwa wa kwenye jela ya Abu Ghraib nchini Iraq.
Bw.
Crowley anasema ikiwa wataendelea na mpango wa kuchoma Quraani, basi
anatumai kuwa watu duniani kote watatambua kuwa kitendo hicho
hakiashirii maoni ya wamarekani wengi na wala utamaduni wa Marekani wa
ustahmilivu wa kidini.
“Ikiwa
jumuiya hii itasonga mbele na mipango yake Jumamosi hii, basi
tunatumai kuwa ulimwengu hauta tuhukumu kutokana na vitendo vya padre
mmoja na wafuasi wake 50, lakini watatuhukumu kulingana na utamaduni
wetu ulionza tangu kubuniwa kwa taifa hili. Hatukuishtaki nchi nzima au
dini yote kutokana na vitendo vya September 11 . Na, tunatumai kuwa
ulimwengu hautoilaumu Marekani kutokana na vitendo vya kikundi kimoja tu
huko Florida,” alisema Bw. Crowley.
Padri
huyo wa Florida anasema anazingatia onyo kuhusu uwezekano wa kutokea
kwa ghasia dhidi ya wamarekani nje ya nchi, lakini anasema yeye pamoja
na wafuasi wake wameshaamua kuwa wataendelea na maandamano yao.
Anasema serikali ya Marekani inafaa kuwaonya waislamu nje ya nchi dhidi ya kufanya kisasi.
0 comments:
Post a Comment