Ikulu ya Marekani yalaani mipango ya kuchoma Koran
WASHINGTON
Ikulu
ya Marekani imeungana na makundi mengine yanayolaani mipango ya Kanisa
moja nchini Marekani kutaka kuchoma moto Koran tarehe 11 ya mwezi huu wa
Septemba.Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Eric Holder ameiita mipango hiyo
kuwa ni ya ''kipumbavu na ya hatari.''Kamanda wa majeshi ya Marekani na
Jumuiya ya Kujihami ya NATO nchini Afghanistan, Jenerali David
Petraeus, alisema mipango ya Kanisa hilo la Florida kutaka kuchoma moto
nakala za kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislamu inaweza ikahatarisha
maisha ya wanajeshi wa Marekani.Wiki chache zilizopita viongozi katika
idara ya moto walitupilia mbali ombi la kufanyika sherehe za kuchoma
moto Koran Tukufu katika eneo la wazi.
0 comments:
Post a Comment