Watu zaidi ya 100 wanahofiwa kupoteza maisha kufuatia maporomoko ya ardhi huko Guatemala.
Duru zinaarifu kuwa hadi sasa miili 23 tayari imeshafukuliwa katika eneo la maafa hayo mjini Santa Maria Ixtaguacan.
Wale waliozikwa hai Jumapili walikuwa wakijaribu kuwaokoa wahanga wengine wa maporomoko ya ardhi ambayo yalipelekea abiria 12 wa basi kupoteza maisha.
Serikali ya Guatemala imesema karibu watu 45 wamepoteza maisha katika maporomoka ya ardhi yaliyosababishwa na mafuriko katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati. Rais Alvaro Colom wa Guatemala ametangaza maporomoka hayo kuwa maafa ya kitaifa.
0 comments:
Post a Comment