SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, September 6, 2010

Magari yateketea moto katika msongamano nchini Nigeria


Fuel tankers, buses ablaze in Nigeria road crash
Moto umezuka katika barabara moja nchini Nigeria kufuatia msongamano mkubwa wa makumi ya magari yakiwemo matrela matatu yaliyokuwa yamesheheni petroli.
Ripoti kutoka jimbo la Ogun zinasema kuwa trela moja la petroli lilipoteza muelekeo na kushika moto ulioenea katika magari mengine yaliyokuwa karibu.
Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Olumuyiwa Adejobi amesema hadi sasa hakuna ripoti za watu kupoteza maisha katika tukio hilo.
Itakumbukwa kuwa mwezi Agosti katika eneo hilo hilo watu 40 walipoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari 20.
Kwa mujibu wa Halmashauri ya Usalama Barabarani Nigeria, kati ya mwaka 2007 hadi 2009 watu zaidi ya 17 elfu walipoteza maisha katika ajali za barabarani nchini humo. 

0 comments:

Post a Comment