Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa wapenda amani duniani kuanzisha mfumo bora unaofaa na kuongeza kuwa mabadiliko katika muundo wa Umoja wa Mataifa yanapaswa kuwa hatua ya kwanza katika harakati hiyo.
Akizungmza na mabalozi wa nchi za kigeni alipokuwa katika safari ya siku moja nchini Qatar Jumapili, Rais Ahmadinejad amesema mfumo wa sasa duniani umejengeka katika msingi wa kulinda maslahi ya madola ya kibeberu na kwamba ni natija ya vita vikuu vya kwanza na vya pili duniani. Amesema mfumo wa sasa wa kimataifa haujaweza kumletea mwanaadamu amani na usalama endelevu na kusema mfano wa hilo ni kushindwa kutatuliwa mgogoro wa Palestina na Wazayuni katika kipindi cha miaka 60 iliyopita. Rais wa Iran amesema kuanzishwa mfumo mpya wa utawala duniani ni jambo linaloweza kumletea mwanaadamu ustawi halisi na kuhitimisha mauji ya halaiki.
0 comments:
Post a Comment