Wapiganaji wa Al Shabaab waapa kufanya mashambulio zaidi.
Wapiganaji wa al Shabaab ambo wameapa kufanya mashabulio zaidi.
Kundi la waasi wa al-Shabaab nchini
Somalia, linalodaiwa kuwa na mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al
Qaeda limeapa kufanya mashambulio zaidi, baada ya kukiri kuhusika na
shambulio lililotokea nchini Uganda.
Kiongozi wa kundi hilo la al Shabaab Mohamed Abdi Godane
ambaye pia anajulikana kama Abu Zubairy alisema katika ujumbe
uliotangazwa na radio za nchi hiyo, kwamba shambulio hilo la
kampala ni mwanzo tu, na kuongeza kuwa watalipiza kisasi dhidi ya
mashambulio yaliyofanywa na kikosi cha Jeshi la Kulinda amani cha
Umoja wa Afrika -AMISOM nchini Somalia na kusababisha vifo vya
raia.
Kundi hilo tayari limekiri kwamba shambulio hilo ni kulipiza kisasi
ya
kuwepo kwa kikosi cha Uganda katika kikosi hicho cha AMISOM,
nchini Somalia.
Al shabaab mara kwa mara limekuwa likitishia kufanya mashambulio
katika eneo hilo la Afrika, lakini shambulio la Uganda ni la kwanza
kufanywa nje ya Siomalia.
Aidha amesema kuwa shambulio hilo la Kampala limefanywa na
kikosi cha wapiganaji hao wa al Shabaab cha Saleh Nabhan, baada
ya mtuhumiwa katika shambulio lililotokea Mombasa mwaka 2002
dhidi ya Israel, ambaye ni mwanachama wa al Qaeda mwenye asili
ya Kenya, kuuawa katika shambulio la anga lililofanywa na marekani
mwaka uliopita.
Wakati al Shabaab wakiapa kuendelea kufanya mashambulio,
Uganda imesema inaweza kupeleka tena kikosi cha wanajeshi 2,000
wanaohitajika, katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani
nchini Somalia.
Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye amesema nchi yake
inaweeza ikachangia wanajeshi hao ama zaidi katika jeshi hilo la
Umoja wa Afrika iwapo nchi nyingine zitashindwa kufanya hivyo.
Akizungumzi jana kuhusiana na kikosi hico Rais Museveni alisema
IGAD itaongeza wanajeshi.
Wakati mkutano wa Umoja wa Afrika ukitarajiwa kufanyika wiki ijayo
nchini Uganda, mataifa wanachama wa umoja huo yameelezwa
kushindwa kutimiza ahadi zao za kuchangia wanajeshi katika kikosi
hicho.
Kikiwa na wanajeshi wachacche zaidi ya elfu saba, kikosi hicho cha
AMISOM kimeweza kwa kiasi kuwepo mpaka sasa kwa serikali ya
mpito unayoungwa mkono na nchi za magharibi ambayo
inaoongozwa na Rais Sharif Sheikh Ahmed, lakini jeshi hilo
limeshindwa kuwamaliza nguvu wapiganaji nchini humo.
Katika hotuba yake jana Rais Musseveni alizitaka nchi za Afrika
kupeleka wanajeshi wake katika jeshi hilo ili kuliongeza na kufikia
kikosi cha wanajeshi elfu 20, na kwamba kwa kushirikiana na serikali
hiyo ya mpito ya Somalia kuweza kuwamaliza magaidi nchini humo.
Wakati huohuo wachunguzi wa Uganda kuhusiana na shambulio la
kigaidi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopta, bado wanaendelea
kuchunguza mazingira ya shambulio hilo la mjini Kampala na
kuwatambua watu waliouawa..
Mwandishi: Halima Nyanza(afp)
0 comments:
Post a Comment