SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 15, 2010

Noorah aingia Mkataba na B-Hits
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Noorah  a.k.a baba styles  aliyepata kutamba na kibao chake cha ice creem ambacho ndicho kilichomtambulisha kwenye gem huku katika kibao hicho akiwa amemshirikisha Suma Lee kutoka kundi la park lane (kipindi kile)
Noora ambaye pia ni msomi wa mambo ya (IT) Information Technology kutoka katika chuo kikuu cha IFM aliiambia Bongo5
kuwa sasa hivi ameamua kurudi upya kwenye gemu kwa miguu yote miwili kwani ameshajipanga vya kutosha kabisa na ameshafanya ngoma kibao ambazo anatarajia kuziachia hivi karibuni huku akiwa amejikita katika katika studio za B Hits pande za namanga namtayarishai wa ngoma zake akiwa ni Pancho Latino.
“Nimejipanga vya kutosha kwani hapa nikisimama mimi mwnyewe, pale akisimama Pancho na kule akisimama mtumzima Hammy B naimani mambo yatakuwa yamesimama maana hii combination sio ya kitoto” alisema Noora.
Kwa upande mwingine Noorah ameweza kushirikiana vyema na mtu mzima Albart Mangwea katika ngoma ambayo ameiachia “katika hii project nimeweza kushirikiana vizuri na mwanangu Ngwea ambaye amefanya mambo kwenye hii ngoma”.
Kuhusu wasanii wangine Noorah alisema wala hawamtishi kitu chochote kwa sababu ya kile alichosaema kuwa  yeye ndio baba style hivyo anabadlika kutokana na wakati na mazingira. “mimi ujio wangu huu utakuwa utakuwa ni wa ukweli kutokana na nimebadilika kabisa na nimeenda na wakati uliopo japo huwa jamii hainelewi kwa haraka ila sasa hivi naamini nitaeleweka tu”.
Noorah kwa sasa amejikita katika muziki na akiwa chini ya studio za B hits…
**************************
MABESTE msanii anayekuja kwa kasi
Jamaa ni mkali ile mbaya kwa jina anaitwa William Ngowi lakini kwa jina la kisanii jamaa anajulikana kama Mabeste kutoka pande za B hits. Mshikaji tuko deep sana kiasi naweza sema akija kusikika hutojutia kumsikiliza tena na tena. Bongo5 haikua nyuma kumtafuta mitaa ya B hits chini ya producer wake Pancho latino. Jamaa anatokea pande za Kenya, Mombasa baada ya kukutana na Pancho latino na kugundua kipaji cha mshikaji pancho hakutaka kumuacha aite mbele yake bila kugusa kinanda na kutoa track ya inayokwenda kwa jina la Nawapenda wakati huo wako Dhahabu Records kwa mtu mzima Dully Sykes.
Mabeste akiwa Chini ya dhahabu records enzi zile haikua tu nawapenda but kama unakumbuka ile Dhabu Anthem track ambayo alikuwepo Dully Mwenyewe, Chidi Beenz, Chiku Ketto, MwanaFA, Mr Blue, Pia Mabeste akuishia hapo Jose Chamilion aliwahi kumtamani pia na wakafanya kazi pamojah.
Baada ya Pancho kutoka Dhahabu Ilibidi mabeste kurudi kenya kwa muda kwa sababu pancho hakutakiwa kuingia na msanii zaidi ya waliopo Kiri Records kipindi hicho.
Pancho hakudumu sana Kiri akaama B hits Groups kwa mtu mzima Hermy B ndipo Mabeste alipopata mwanya tena wa kurudi Bongo na hakusita kutoa track moja matata inayokwenda kwa jina la Nacheza Raff,ambayo haikuweza fanya vizuri, Pesa Iko wapi ambayo amemshirikisha Amani, Sukuma.
Na sasa Mabeste Ameachia Track yake mpya inyokwenda kwa jina la chupa Moja produza akiwa na Pancho latino toka B hits.

0 comments:

Post a Comment