KIJANA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI JIJINI
DAR ES SALAAM MCHANA KWEUPE!!
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sadam
ameauwa kwa kupigwa risasi mchana wa jana katika baa maarufu ya Angels'
Park iliyoko Ilala Sharief Shamba jijini Dar es salaam!! Kijana huyo
inadaiwa kuuawa na mmiliki wa bar hiyo baada ya kundi la vijana wengi,
akiwemo marehemu, kuvamia kwa lengo la kumpiga mwenye baa ili kulipiza
kisasi! Mtandao huu umeeleza na mashuhuda kuwa, sakata lilianzia jana
baada ya vijana wasiojulikana kudaiwa kumkaba mteja mmoja wa baa hiyo
akiwa chooni na vijana hao kukamatwa na kuplekwa polisi ambako
walishikiliwa hadi leo. Imedaiwa kuwa baada ya kuona wenzao wanasota
rumande, pengine kwa sababu ya mmiliki wa huyo, waliamua kumfuata ili
kulipiza kisasi kwa kumfanyia.
Wakiwa kundi huku wameshika silaha mbalimbali vikiwemo visu, vijana hao
walivamia baa hiyo na kuanza kumpiga mwenye baa na kumchoma kisu ambacho
bahati nzuri hakikumdhuru sana. Kuona hali hiyo, mwenye baa alitoa
bastola yake, akapiga hewani ili kuwatisha, lakini waliendelea kumfuata
na kumshambulia huku wakiharibu mali za baa hiyo, likiwemo gari lake
lililovunjwa kioo cha nyuma. Awali vijana wawili walipigwa risasi na
kujeruhiwa na marehemu aliendelea kumfuata mwenye baa na ndipo
alipopigwa risasi na kufa papo hapo!
Habari na www.globapublisherstz.com
0 comments:
Post a Comment