SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 15, 2010

Shahram Amiri awasili Tehran, Iran yasema, si mtaalamu wa nyuklia
Sample ImageShahram Amiri, mhadhiri wa Chuo Kikuu nchini Iran aliyekuwa ametekwa nyara na Marekani na kudaiwa ni mtaalamu wa nyuklia, amerejea hapa Tehran mapema leo Alkhamisi na kupokewa na Naibu Waziri wa Elimu, Utafiti na Teknolojia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini (MA).
Mwandishi wa Radio Tehran ameripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, juzi Jumanne, Amiri alipelekwa kwenye ubalozi wa Pakistan mjini Washington ambao ndio unaolinda maslahi ya Iran nchini Marekani akisisitizia msimamo wake wa kutaka kurejea nchini.
Wakati huo huo Bw. Javad Jahangizadeh, mjumbe katika Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amesema kuwa, Marekani ilifanya kosa kubwa kumteka nyara Shahram Amiri na haikuwa na njia nyingine ila kumwachilia huru baada ya kubainika kosa hilo la aibu lililotokana na taarifa ghalati za kijasusi.
Aidha amesema vitendo vya kijasusi vya utawala wa Kizayuni vinaonekana wazi katika ndchi za Kiislamu na kuongeza kuwa, bila ya shaka yoyote utawala wa Kizayuni unashirikiana bega kwa bega na Marekani katika vitendo vya kijasusi dhidi ya Iran.
Mara baada ya kuwasili hapa mjini Tehran, Amiri amesema atafichua zaidi jinsi alivyotekwa nyara nchini Saudi Arabia alikokwenda kufanya amali ya Umra, na baadaye kupelekwa Marekani.
Katika upande mwingine, Bw. Hasan Qashqavi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya balozi, masuala ya bunge na masuala Wairani waishio nje ya nchi leo Alkhamisi amekanusha madai ya vyombo vya habari kuwa Amiri ni mtaalamu wa nyuklia.
Vile vile amesema kurejea mhadhiri huo wa Chuo Kikuu nchini Iran hakuna uhusiano wowote na suala la Wamarekani watatu waliotiwa mbaroni nchini Iran baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria.

0 comments:

Post a Comment