Mamia ya waombolezaji
wamehudhuria mazishi ya mtetezi mkuu wa haki za binadamu wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Floribert Chebeya, aliyeuliwa mapema mwezi huu.
Zaidi ya watu elfu moja, akiwemo waziri wa
sheria na haki za binadamu wa nchi hiyo, Bambi Luzolo, pamoja na
mabalozi wa mataifa ya nchi za magharibi, walihudhuria ibada katika
kanisa moja mjini Kinshasa.
Floribert Chebeya alipatikana akiwa ameuawa
ndani ya gari lake mwanzoni mwa mwezi huu.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini
Congo yalitaka maziko yafanyike siku ya kimataifa ya kuwakumbuka
walionyanyaswa na kuteswa, ili wengi waweze kumkumbuka vyema Chebeya.
Bw Chebeya aliongoza kampenzi za kutetea haki za
binadamu nchini Congo, kwa muda wa miongo mitatu iliyopita.
Licha ya kutaka uchunguzi huru ufanyike kufuatia
kifo chake, tume moja ya kijeshi imepewa jukumu hilo.
Viongozi kadhaa wa upinzani walikusanyika nje ya
kanisa, wakitaka Rais Joseph Kabila ajiuzulu.
0 comments:
Post a Comment